Biriani Ya Tuna

Biriani Ya Tuna

 

 

 

VIPIMO

 

 

Mchele Basmati - Mugs 2 ½

Vitunguu (Vikubwa kiasi) - 3

Tuna - Vibati 3

Carrot - 2 kubwa

Tomatoe paste - 1 kikopo

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 2 Vijiko vya supu

Tangawizi - 2 Vijiko vya supu

Uzile  (Bizari ya pilau ya unga) (cummin powder )

(Jeera) - ½ Kijiko cha supu

Mdalasini - ½ Kijiko Cha supu

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

Tuna carrots (grate) ziwe kama chicha  weka kando.

Kaanga vitunguu 2 mpaka viwe brown weka pembeni.

Kaanga Kitunguu cha 3 halafu changanya na tangawizi, thomu, na tuna huku unakoroga.

Changanya na tomatoe, uzile (cummin powder) na mdalasini, koroga vizuri (hakikisha umeweka mtoto mdogo mdogo kwani ni rahisi kuungua) 

Ikiwiva  epua weka pembeni.

Chemsha wali wako kwa maji mengi na uuchuje kabla haujawiva vizuri na uugawe sehemu

Chukua trey au sufuria ambayo itaweza kuingia vitu vyote uilivyoandaa, tandaza fungu la kwanza  la wali halafu utandaze carrot juu yake.

Tandaza fungu la pili la wali halafu utandaze vitunguu juu yake.

Tandaza fungu la tatu la wali halafu utandaze  tuna (masalo) juu yake.

Mwisho tandaza fungu la nne la wali,  ufunike vizuri na upike kwenye oven (bake)  350 Deg C kwa muda wa dakika 20

Epua ikiwa tayari kuliwa

 

Share