Skip navigation.
Home kabah

Keki Za Vikombe



Vipimo

 

Unga wa ngano                       vikombe 2-3

Mayai                                      6

Maziwa                                    kikombe 1

Sukari                                      kikombe 1

Siagi                                        kikombe 1

Baking powder                        vijiko vya chai 2-3 (kijiko 1 kwa kikombe cha unga 1)

Vanilla                                      kijiko cha chai 1

Rose essence                          kijiko cha chai robo(kiasi unavyotaka harufu ijitokeze)

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

1.  Saga siagi, sukari, mayai na essence ya vanilla na rose

2.  Ikishasagika tia unga na maziwa koroga tena.

3.  Mwisho tia baking powder na koroga mpaka ichanganyike.

4.  Washa oven lako moto wa 350’F kwa dakika 2-3.

5.  Chukua treya maalum ya kupikia cupcakes / muffins, tia karatasi za duara maalum za kupikia keki hizi kwenye kila duara la treya.(huna haja ya kupaka mafuta kwenye treya)

6.  Kisha tumia kijiko kikubwa chota mchanganyiko huo wa keki na tia ndani ya karatasi hizo za duara kiasi cha robo tatu (3/4) yaani usijaze mpaka juu.

7.  ukimaliza kuvijaza vyote tia kwenye oven kwa muda wa dakika 20 – 25.

8.  zitoe panga kwenye sahani ziache zipoe kidogo na tayari kuliwa na chai au kuwafungia watoto shuleni kama snack.