Nasiha Na Ukumbusho: Swawm Tarehe 9 Na 10 Al-Muharram Inafuta Madhambi Ya Mwaka Mzima!
Nasiha Na Ukumbusho Wa Swawm
Siku Ya Taasu'aa (9) Na 'Aashuraa (10)
Nasiha: Swiyaam Tarehe 9 na 10 Al-Muharram zimesisitizwa na fadhila zake ni kufutiwa madhambi ya mwaka mzima; Nazo zitakuwa ni kama ifuatavyo:
9 Al-Muharram (Taasu'aa)
10 Al-Muharram ('Aashuraa)
Asiyejaaliwa kuunganisha Swawm tarehe 9 pamoja na tarehe 10, basi aunganishe tarehe 10 na tarehe 11. Na asiyejaaliwa vyovyote hivyo, basi asikose Swawm ya tarehe 10 Al-Muharram pekee.
Bonyeza viungo vifuatavyo upate faida tele kuhusiana na Fadhila Za Mwezi wa Al-Muharram na Swiyaam zake:
Fadhila Za Mwezi Wa Al-Muharam Na Siku Ya 'Aashuraa Na Bid'ah Zake
Fadhila Za Swiyaam Za Fardhi Na Za Sunnah
Wa biLLaahi At-Tawfiyq
