08-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Hikma Ya Kujizuia Kukata Nywele, Kucha Kwa Mwenye Kunuia Kuchinja

 

Hikma Ya Kujizuia Kukata Nywele, Kucha Kwa Mwenye Kunuia Kuchinja

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Ni ipi hekima kwa anayetaka kufanya Udhwhiya kujizuia kukata nywele zake, kucha na kutoa kitu katika ngozi?

 

 

JIBU:

 

 

a-Miongoni mwa neema za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  kwa waja Wake ni kuwa pindi wanapoondoka watu kwenye kuhiji na kufanya ‘ibaadah na kuacha waliyoacha ni kuwa Allaah Amewaamrisha waliobaki kushirikiana na Hujaji kwa kuacha kufanya baadhi ya mambo kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allaah.

 

 

b-Mchinjaji anashirikiana na Hujaji katika baadhi ya matendo ya ‘ibaadah nayo ni kujikurubisha kwa Allaah kwa kuchinja. Mtu huyu anayetaka kuchinja anashirikiana na Hujaji katika sifa za Ihraam nazo ni kujizuia na kukata nywele na kucha.

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (25/139)]

 

 

Share