09-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Mnyama Yupi Bora Kwa Udhwhiya Aliye Mnene, Mwenye Mafuta Mengi Au Mwenye Thamani?

 

Mnyama Yupi Bora Kwa Udhwhiya Aliye Mnene,

Mwenye Mafuta Mengi Au Mwenye Thamani?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Ni kipi bora katika Udhwhiya? Je, ni mnyama mkubwa wa kiwiliwili mwenye mafuta mengi au mwenye thamani kubwa?

 

 

JIBU:

 

 

Tukiangalia manufaa ya Udhwhiya ni kuwa mnyama mkubwa mwenye nyama nyingi anakuwa ni bora.

 

 

Na tukiangalia ukweli wa kutaabadi kwa ajili ya Allaah ('Azza wa Jalla)  tutasema mwenye thamani kubwa ni bora.

 

Hata hivyo angalia kilicho kizuri zaidi kwa moyo wako na ufanye na ukiona kuwa nafsi yako inazidi iymaan na kujidhalilisha kwa Allaah ('Azza wa Jalla)  kwa kutoa thamani zaidi basi fanya hivyo.

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (25/35)]

 

 

Share