Skip navigation.
Home kabah

Spageti Ya Kuku Na Sosi Za HP Na Soya


 

VIPIMO

 Spaghetti                                                   500 gramu (gms)

Chumvi                                                       Kiasi

Mafuta ya kukaangia                                    1/4 kikombe

Kitungu kilichokatwa                                    1 kiasi

Pilipili ya unga                                               1/2 kijiko cha chai

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa      1 kijiko cha chai

Sosi ya pilipili (HP sauce)                              1 kijiko cha chai

Siki                                                              3 Vijiko vya supu 

Sosi ya soy                                                 3 vijiko vya supu

Pilipili mboga kijani na nyekundu                   1 kila moja (iliyokatwa)

Mchanganyiko wa mboga za barafu             1 magi

Kuku au nyama isio na mifupa iliyokwishapikwa kiasi upendavyo

 

NAMNA  YA  KUTAYARISHA  NA  KUPIKA

 
 
1.       Chemsha spaghetti kwa chumvi na mafuta kidogo kwa kufuata maagizo yake katika karatasi.
 
2.       Yakishawiva mwaga maji kwa kuchuja na uweke kando.
 
3.       Katika sufuria kubwa , tia mafuta na kaanga vitungu , mchanganyiko wa mboga , chumvi na pilipili hadi mboga iive kidogo na sio kuvurujika.
 
4.       Tia na ukaange vilivyobaki isipokuwa spaghetti na kuku unaziwacha mwisho.
 
5.       Iwache dakika 2 hivi kwenye moto mdogo na itakuwa tayari kuliwa.
 

 

Rudi Juu