Skip navigation.
Home kabah

Pai Ya Viazi Na Nyama Ya Kusaga

 

Vipimo

 

Nyama ya kusaga                                      1½ lb (ratili)

Kitunguu                                                   1 Kikubwa

Thomu na tangawizi                                   1 Kijiko cha supu

Mboga upendayo

(karoti, mahindi, na kadhalika)                    1- 2 Kikombe

Viazi                                                          1½ - 2 lb (ratili)

Siagi                                                          ½ Kikombe

Kidonge cha supu kilichoyeyushwa               ½ Kikombe maji

Worcestershire sauce au yoyote nyingine      1 Kijiko

Chumvi                                                      kiasi

Mchanganyiko wa bizari                              1 Kijiko cha supu

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  

1.       Menya maganda ya viazi na katakata, kisha chemsha katika maji yenye chumvi hadi viwive.

2.       Wakati viazi vinaiiva, yeyusha nusu ya ile kipimo cha siagi katika sufuria kisha kaanga kitunguu hadi ilainike.

3.       Kisha tia thomu na tangawizi.

4.       Halafu tia nyama ya kusaga na ukaange hadi isiwe nyekundu tena.

5.       Weka mboga, chumvi na bizari zilizobakia na iachie moto mdogo kwa muda iive vizuri.

6.       Ponda viazi pamoja na ile siagi iliyobakia, kisha ongeza chumvi na pilipili manga ikiwa haijakolea.

7.       Weka mchanganyiko wa nyama katika treya ya oveni kisha tandaza ile viazi vilivyopondwa kwa kutumia uma ili iwe na dizaini upendayo.

8.       Pika katika oveni yenye moto wa 400° kwa muda wa dakika 30 hivi na ubadilisha moto wa juu katika dakika 5 za mwisho ili igeuke rangi ya kupendeza juu.

9.       Epua na tayari kuliwa.