Mahshi Waraqah ‘Anab - Majani Ya Zabibu Yaliyojazwa (Shaam)

Mahshi Waraqah ‘Anab - Majani Ya Zabibu Yaliyojazwa  (Shaam)

 

Vipimo

 

Majani ya Zabibu (Grape leaves) - 1 Kilo

(au yanapatikana katika chupa)

Mchele wa Kimisri (Egyptian rice)

uliooshwa na kuchujwa - 2 Vikombe

(ni mchele wa chembe ndogo ndogo

zaidi kuliko wa kawaida)

Vitunguu maji     vilivyosagwa - 5 

Mafuta - ¼ kikombe

Kotmiri iliyokatwa ndogo ndogo kabisa - ¼ kikombe

Baqdunis (Parsely leaves) iliyokatwa

ndogo ndogo kabisa - ¼ kikombe

Nyanya ya kopo - ½ kibati

Ndimu ya maji - ½ kikombe

Mafuta ya zaituni (olive oil) - ½ kikombe

Viazi vilivyokatwa duara nyembamba - 3

Maji - 3 Vikombe

Bizari ya pilau ya unga  (cumin powder) - ½ kijiko                      

Pilipili manga - ½ kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Kata vishina vya majani ya zabibu, kisha osha na uchemshe kidogo katika maji ya moto.   Na ikiwa ni ya tayari katika chupa, yaoshe vizuri. kama mara tatu ukibadilisha maji ili kutoa chumvi yake, kisha yachemshe katika maji ya moto kwa muda mdogo tu kama dakika 5 kisha yachuje maji.
  2. Tia mafuta ¼ kikombe katika sufuria na kaanga vitunguu kidogo tu kisha epua.
  3. Tia mchele, nyanya ya kopo, pilipili manga, chumvi, bizari na uchanganye vizuri, kisha rudisha katika moto upike kama dakika 5 tu kisha epua.
  4. Tia kotmiri na Baqdunis uchanganye vizuri.
  5. Panga vipande vya viazi katika sufuria chini ili kuzuia kuganda majani ya zabibu.
  6. Fungua jani moja moja la zabibu utie mchanganyiko kisha ufunge kwa kukunja   pande zote mbili kwanza ukiwa unafunika mchanganyiko, kisha zungurusha (Roll) na kukunja jani lote. Hakikisha unabana vizuri unapokujnga.
  7. Panga juu ya viazi kisha tia maji, ndimu ya maji, mafuta ya zaituni, kisha ufunike vizuri sufuria huku uweke kitu juu yake kizito ili maji yasiingie ndani ya sufuria wakati inachemka. (kama unavyopika pudini (pudding)
  8. Pika katika moto mkali kwanza kisha punguza na kuacha moto mdogo mdogo muda wa saa moja, kisha acha ipoe kidogo, fungua utoke mvuke.
  9. Pakua katika sahani  ikiwa tayari.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)

 

 

Share