Shaykh Fawzaan: Wajibu Wetu Kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Na Kukithirisha Kumswalia

 

Wajibu Wetu Kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Na Kukithirisha Kumswalia

 

Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

 

Nini wajibu wetu kwa Rasuli wetu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)? Na je, inatosheleza kumswalia kwa wingi?

 

JIBU:

 

Naam, kumswalia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni katika haki yake kutoka kwetu kutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ ۚ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٥٦﴾

Hakika Allaah na Malaika Wake wanamswalia Nabiy. Enyi walioamini mswalieni na msalimieni kwa maamkizi ya amani na kwa tasliymaa.  [Al-Ahzaab 33: 56]

 

 

 

Na amesema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

((مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلاَةً، صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عشْراً))  رواهُ مسلم

 ((Atakayeniswalia mara moja, Allaah Atamswalia mara kumi)) [Muslim]

 

Hivyo kuna fadhila adhimu nayo ni haki yake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuswaliwa na Ummah wake. 

 

Vile vile kufuata (Sunnah zake) na kufuata kigezo chake  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), na hii ni waajib kwa Muislamu kama Anavyosema Allaah ('Azza wa Jalla):

 

لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ    

Kwa yakini mna kigezo kizuri kwa Rasuli wa Allaah  

 

Yaani mwongozo wake, na…

لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّـهَ كَثِيرًا  

Kwa mwenye kumtaraji Allaah na Siku ya Mwisho na akamdhukuru Allaah kwa wingi. [Al-Ahzaab: 21]

 

 

[Mawqi’  awqi' Ar-Rasmiy li-Ma'aaliy Shaykh Ad-Duktuwr Swaalih bin Fawzaan]

 

Share