Adhabu Si Katika Mwili Mali Na Ahli
Bali Adhabu Mbaya Kabisa Ni Kuwa Na Maradhi Ya Moyo
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah) amesema:
“Watu wengi wanadhania kwamba adhabu inahusiana katika siha ya mtu, afya, mali na watoto, bali kuwa na maradhi ya moyo na moyo uliofisidika ndio adhabi mbaya zaidi.”
[Ahkaam Min-Al-Quraan (1/87)]
Faida: Maradhi ya moyo yaliyokusudiwa ni yale yaliyotajwa katika Qur-aan kama shirki, bid’ah, unafiki, uhusuda, chuki, mafundo na vinyongo na kila aina ya maasi.