Makaroni Ya Bashamella Na Nyama Ya Kusaga

Makaroni Ya Bashamella  Na Nyama Ya Kusaga

Vipimo

Makoroni - 500 gms

Mafuta ya kuchemshia makoroni - ¼ kikombe            

Nyama ya kusaga - ½ kilo

Mafuta - ¼ kikombe

Vitunguu vilivyokatwa (chopped) - 3

Tomato iliyokatwa ndogo ndogo - 1

Pilipili mboga iliyokatwa ndogo ndogo - 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha supu

Pilipili manga - 1 kijiko cha supu

Chumvi - kiasi

Vipimo Vya Bashamela

Unga - 5 vijiko vya supu          

Siagi - 3 vijiko vya supu

Maziwa - 5 vikombe

Jibini (Cheese) Ya Malai (Cream) - 3 vijiko vya supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Makaroni

  1. Chemsha macaroni na mafuta  hadi yawive mwaga maji na chuja.

Sosi Ya Nyama

  1. Kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi.
  2. Tia thomu kaanga kidogo.
  3. Tia nyama, chumvi na pilipili kaanga hadi nyama iwive.
  4. Ukipenda tia mraba wa supu ya nyama - kidonge 1 (au supu yenyewe kiasi kidogo tu cha kutia ladha lakini hakikisha supu isizidishe kipimo kwa kupunguza maji au maziwa).
  5. Zima moto, tia nyanya na pilipili mboga.
  6. Bashamela
  7. Katika sufuria tia siagi weka katika moto.
  8. Tia unga na kaanga ugeuke rangi uwe rangi brauni khafifu.
  9. Tia maziwa na haraka haraka ukoroge kwa mchapo wa mayai kutoa madonge.
  10. Tia cheese.  Ikiwa madonge hayakutoka tia katika mashine ya kusagia (blender) na usage kisha rudisha kidogo katika moto mdogo mdogo na huku unakoroga kwa mchapo wa mayai.

Kutayarisha Kuyapika

  1. Tia nusu ya sosi ya nyama chini ya bakuli la kupikia katika oveni.
  2. Tia nusu makaroni na mwagia nusu ya bashamela.
  3. Tia tena nusu nyingine ya nyama kisha tena makaroni kisha tena bashamela.
  4. Pika (bake) katika moto wa 400 Deg kwa muda wa dakika 15-20 hadi bashamela igeuke rangi kidogo.
  5. Epua ikiwa tayari kuliwa.
 
 
 

 

 

 

 

 

Share