Macaroni Ya Express Ya Kidari Cha Kuku

Macaroni Ya Express Ya Kidari Cha Kuku Na Jibini

Vipimo

Makaroni - 500 gm

Kidari cha kuku katakata vipande - ½ kilo                        

Kitunguu katakata kidogodogo - 1

Nyanya/tungule katakata ndogo ndogo - 3

Thomu (garlic) ilosagwa - 1 kijiko cha chai

Nyanya kopo (paste) - 1 kijiko cha kulia

Pilipili nyekundu ya unga - ½ kijiko cha chai

Mafuta ya kupikia - 3 vijiko cha kulia

Jibini (Cheese) iliyokunwa ya cheddar - ½ kikombe

 Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  

  1. Weka mafuta katika sufuria yakishika moto kaanga vitunguu mpaka vilainike.
  2. Tia thomu (kitunguu saumu) endelea kukaanga kwa dakika moja.

  3. Tia kuku, chumvi, pilipili na endelea kukaanga au kukoroga. Acha ipikike bila kuifunika mpaka kuku aive.

  4. Tia nyanya, changanya ukoroge mpaka nyanya ziive na kuwa laini kisha tia nyanya kopo.

  5. Tia macaroni, koroga, kisha tia maji kiasi yafunike macaroni. Koroga kisha funika na punguza moto uwe mdogo.

  6. Pika kwa dakika 15, koroga kisha tazama kama macaroni yameiva na maji yamekauka. Yakiwa hayakuiva bado ongezea maji lakini yasizidi ¼ kikombe. Na yakiwa yameiva na bado yana maji, funua mfuniko upike wazi ili maji yakauke.

  7. Zima moto, kisha changanya na jibini (cheese) kisha pakua katika chombo yakiwa tayari.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

 

Share