Keki Ya Karoti

Keki Ya Karoti

Vipimo

Unga - 1 Kikombe cha chai

Baking soda - 1 Kijiko cha chai

Iliki ya unga -   ½ Kijiko cha chai

Chumvi -   ½ Kijiko cha chai

Mayai -   2

Mafuta -   ¼ Kikombe cha chai

Sukari -  ½ Kikombe cha chai

Sukari ya hudhurungi (brown sugar) -  Kikombe cha chai        
Mtindi (yogurt) -  Kikombe cha chai

Karoti iliyokaruzwa -  1 Kikombe cha chai (kama karoti 2)

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Washa oveni moto wa 350°F.  
  2. Paka mafuta chombo utakayopikia keki, kisha nyunyiza unga na gonga iliyozidi.  
  3. Kwenye bakuli la kiasi, changanya pamoja unga, baking soda, iliki, na chumvi weka kando.  
  4. Katika bakuli nyengine, piga mayai, sukari, mtindi, na mafuta mpaka ilainike.
  5. Polepole changanya mchanganyiko wa mayai kwenye wa unga hadi ilainike; kisha tia karoti.  
  6. Mimina kwenye chombo uliyo tayarisha na uvumbike kwa dakika 40 - 45.  
  7. Kisha iache ipoe kwenye sufuria dakika 15 halafu pindua na iache ipoe kabisa.  
  8. Tengeneza sukari laini (icing sugar) ½ kikombe na vijiko 2 vya maji na unyunyizie juu; na ikisha kauka itakuwa tayari kuliwa.

 

 

Share