043-Az-Zukhruf

 

  الزُّخْرُف

 

043-Az-Zukhruf

 

043-Az-Zukhruf: Utangulizi Wa Suwrah

 

 Alhidaaya.com 

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

حم﴿١﴾

1. Haa Miym.[1] 

 

 

وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ﴿٢﴾

2. Naapa kwa Kitabu (Qur-aan) kinachobainisha.

 

 

 

إِنَّا جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ﴿٣﴾

3. Hakika Sisi Tumekifanya kisomeke kwa Kiarabu ili mpate kutia akilini.

 

 

 

 

وَإِنَّهُ فِي أُمِّ الْكِتَابِ لَدَيْنَا لَعَلِيٌّ حَكِيمٌ﴿٤﴾

4. Na hakika hii (Qur-aan) iko Kwetu katika Mama wa Kitabu[2] Imetukuka kwa hakika, imejaa hikmah.

 

 

 

أَفَنَضْرِبُ عَنكُمُ الذِّكْرَ صَفْحًا أَن كُنتُمْ قَوْمًا مُّسْرِفِينَ﴿٥﴾

5. Je, Tuwaondoshelee mbali Ukumbusho huu kwa vile nyinyi mmekuwa wapindukao mipaka?[3]

 

 

 

وَكَمْ أَرْسَلْنَا مِن نَّبِيٍّ فِي الْأَوَّلِينَ﴿٦﴾

6. Na Manabii wangapi Tumewatuma kwa watu wa awali?

 

 

 

 

وَمَا يَأْتِيهِم مِّن نَّبِيٍّ إِلَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ﴿٧﴾

7. Na hakuwafikia Nabiy yeyote isipokuwa walikuwa wakimfanyia istihzai.

 

 

 

 

 

فَأَهْلَكْنَا أَشَدَّ مِنْهُم بَطْشًا وَمَضَىٰ مَثَلُ الْأَوَّلِينَ﴿٨﴾

8. Basi Tukawaangamiza walio na nguvu zaidi kuliko wao, na umeshapita mfano wa watu wa awali.

 

 

 

 

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ خَلَقَهُنَّ الْعَزِيزُ الْعَلِيمُ﴿٩﴾

9. Na ukiwauliza:  Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi? Bila shaka watasema: Ameziumba Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote.[4]

 

 

 

الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ مَهْدًا وَجَعَلَ لَكُمْ فِيهَا سُبُلًا لَّعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ﴿١٠﴾

10. Ambaye Amekufanyieni ardhi kuwa tandiko, na Akakufanyieni humo njia ili msipotee muendako.

 

 

 

 

وَالَّذِي نَزَّلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً بِقَدَرٍ فَأَنشَرْنَا بِهِ بَلْدَةً مَّيْتًا ۚ كَذَٰلِكَ تُخْرَجُونَ﴿١١﴾

11. Na Ambaye Ameteremsha kutoka mbinguni maji kwa kadiri ya kipimo, Tukafufua kwayo nchi iliyokufa, na hivyo ndivyo mtakavyotolewa.[5]

 

 

 

 

 

وَالَّذِي خَلَقَ الْأَزْوَاجَ كُلَّهَا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ الْفُلْكِ وَالْأَنْعَامِ مَا تَرْكَبُونَ﴿١٢﴾

12. Na Ambaye Ameumba kila kitu jozi; dume na jike, na Akakufanyieni mnavyovipanda kati ya merikebu na wanyama.

 

 

 

 

 

لِتَسْتَوُوا عَلَىٰ ظُهُورِهِ ثُمَّ تَذْكُرُوا نِعْمَةَ رَبِّكُمْ إِذَا اسْتَوَيْتُمْ عَلَيْهِ وَتَقُولُوا سُبْحَانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَـٰذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِينَ﴿١٣﴾

13. Ili mlingamane sawasawa juu ya mgongo wake, kisha mkumbuke Neema ya Rabb wenu mtakapolingamana sawasawa juu yao, na mseme:[6] Utakasifu ni wa (Allaah) Ambaye Ametutiishia haya, na tusingeliweza wenyewe kumdhibiti.

 

 

وَإِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا لَمُنقَلِبُونَ﴿١٤﴾

14. Na hakika kwa Rabb wetu, bila shaka tutarejea.

 

 

 

 

وَجَعَلُوا لَهُ مِنْ عِبَادِهِ جُزْءًا ۚ إِنَّ الْإِنسَانَ لَكَفُورٌ مُّبِينٌ﴿١٥﴾

15. Na wakamfanyia kati ya Waja Wake sehemu (kuwa Allaah Ana watoto).[7] Hakika   binaadam bila shaka ni mwingi wa kukufuru, bila kuficha ukafiri wake.

 

 

 

 

أَمِ اتَّخَذَ مِمَّا يَخْلُقُ بَنَاتٍ وَأَصْفَاكُم بِالْبَنِينَ﴿١٦﴾

16. Je, Amejichukulia katika Aliowaumba mabanati[8], na Akakukhitarieni nyinyi watoto wa kiume?

 

 

 

وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُم بِمَا ضَرَبَ لِلرَّحْمَـٰنِ مَثَلًا ظَلَّ وَجْهُهُ مُسْوَدًّا وَهُوَ كَظِيمٌ﴿١٧﴾

17. Na anapobashiriwa mmoja wao kwa yale aliyompigia mfano Ar-Rahmaan (binti), husawijika uso wake, naye ni mwenye kuzuia ghadhabu na huzuni.[9]

 

 

 

أَوَمَن يُنَشَّأُ فِي الْحِلْيَةِ وَهُوَ فِي الْخِصَامِ غَيْرُ مُبِينٍ﴿١٨﴾

18. Ah! (Wanampendelea Allaah kiumbe) aliyelelewa katika mapambo naye katika mabishano si mbainifu?!

 

 

 

 

 

وَجَعَلُوا الْمَلَائِكَةَ الَّذِينَ هُمْ عِبَادُ الرَّحْمَـٰنِ إِنَاثًا ۚ أَشَهِدُوا خَلْقَهُمْ ۚ سَتُكْتَبُ شَهَادَتُهُمْ وَيُسْأَلُونَ﴿١٩﴾

19. Na wakawafanya Malaika ambao ni Waja wa Ar-Rahmaan kuwa ni wa kike.[10] Je, kwani wameshuhudia uumbaji wao?  Utaandikwa ushahidi wao, na wataulizwa.

 

 

 

 

وَقَالُوا لَوْ شَاءَ الرَّحْمَـٰنُ مَا عَبَدْنَاهُم ۗ مَّا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنْ عِلْمٍ ۖ إِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ﴿٢٠﴾

20. Na wakasema: Angelitaka Ar-Rahmaan tusingeliyaabudu (miungu ya uongo). Hawana ilimu yoyote ya hayo, hawana isipokuwa wanabuni uongo.

 

 

 

 

أَمْ آتَيْنَاهُمْ كِتَابًا مِّن قَبْلِهِ فَهُم بِهِ مُسْتَمْسِكُونَ﴿٢١﴾

21. Au Tumewapa Kitabu kabla yake (hii Qur-aan), basi wao kwacho wanakishikilia?

 

 

 

 

بَلْ قَالُوا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَىٰ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰ آثَارِهِم مُّهْتَدُونَ﴿٢٢﴾

22. Bali wamesema: Hakika sisi tumewakuta baba zetu juu ya dini, na hakika sisi tunajiongoza kwa kufuata nyayo zao.[11]

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ مَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ فِي قَرْيَةٍ مِّن نَّذِيرٍ إِلَّا قَالَ مُتْرَفُوهَا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَىٰ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰ آثَارِهِم مُّقْتَدُونَ﴿٢٣﴾

23. Na hiyo ndiyo hali yao, kwani Hatukutuma kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika mji mwonyaji yeyote yule isipokuwa walisema matajiri wake wenye starehe na taanusi: Hakika sisi tumewakuta baba zetu juu ya dini, na hakika sisi ni wenye kufuata nyayo zao.

 

 

 

 

قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكُم بِأَهْدَىٰ مِمَّا وَجَدتُّمْ عَلَيْهِ آبَاءَكُمْ ۖ قَالُوا إِنَّا بِمَا أُرْسِلْتُم بِهِ كَافِرُونَ﴿٢٤﴾

24. (Kila Rasuli) alisema: Japo hata kama nimekujieni na uongofu zaidi kuliko ambao mmewakuta nao baba zenu? Wakasema: Hakika sisi tunayakanusha yale mliyotumwa nayo.

 

 

 

فَانتَقَمْنَا مِنْهُمْ ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ﴿٢٥﴾

25. Basi Tukawalipizia. Hebu tazama vipi ilikuwa hatima ya wenye kukadhibisha!   

 

 

 

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ إِنَّنِي بَرَاءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ﴿٢٦﴾

26. Na pale Ibraahiym alipomwambia baba yake na kaumu yake: Hakika mimi nimejitoa katika dhima na yale mnayoyaabudu.

 

 

 

إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّهُ سَيَهْدِينِ﴿٢٧﴾

27. Isipokuwa kwa Ambaye Ameniumba, basi hakika Yeye Ataniongoza.

 

 

 

 

وَجَعَلَهَا كَلِمَةً بَاقِيَةً فِي عَقِبِهِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ﴿٢٨﴾

28. Na akalifanya neno (laa ilaaha illaa-Allaah) lenye kubakia katika kizazi chake ili wapate kurejea.

 

 

 

بَلْ مَتَّعْتُ هَـٰؤُلَاءِ وَآبَاءَهُمْ حَتَّىٰ جَاءَهُمُ الْحَقُّ وَرَسُولٌ مُّبِينٌ﴿٢٩﴾

29. Bali Niliwastarehesha hawa (makafiri wa Makkah) na baba zao mpaka ikawajia haki na Rasuli anayebainisha.

 

 

 

 

وَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ قَالُوا هَـٰذَا سِحْرٌ وَإِنَّا بِهِ كَافِرُونَ﴿٣٠﴾

30. Na ilipowajia haki, walisema: Hii ni sihiri, na hakika sisi ni wenye kuikanusha.

 

 

 

 

وَقَالُوا لَوْلَا نُزِّلَ هَـٰذَا الْقُرْآنُ عَلَىٰ رَجُلٍ مِّنَ الْقَرْيَتَيْنِ عَظِيمٍ﴿٣١﴾

 

31. Na wakasema: Kwa nini isiteremshwe hii Qur-aan kwa mtu adhimu kutoka miji miwili?[12] 

 

 

 

 

أَهُمْ يَقْسِمُونَ رَحْمَتَ رَبِّكَ ۚ نَحْنُ قَسَمْنَا بَيْنَهُم مَّعِيشَتَهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَرَفَعْنَا بَعْضَهُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَاتٍ لِّيَتَّخِذَ بَعْضُهُم بَعْضًا سُخْرِيًّا ۗ وَرَحْمَتُ رَبِّكَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ﴿٣٢﴾

32. Je, wao wanazigawanya Rehma za Rabb wako? Sisi Tumegawanya baina yao maisha yao katika uhai wa dunia, na Tukawanyanyua baadhi yao juu ya wengineo kwa daraja ili watumikishane wao kwa wao. Na Rehma za Rabb wako ni bora kuliko wanayoyajumuisha.

 

 

 

 

 

وَلَوْلَا أَن يَكُونَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً لَّجَعَلْنَا لِمَن يَكْفُرُ بِالرَّحْمَـٰنِ لِبُيُوتِهِمْ سُقُفًا مِّن فِضَّةٍ وَمَعَارِجَ عَلَيْهَا يَظْهَرُونَ﴿٣٣﴾

33. Na lau isingelikuwa watu watakuwa ummah mmoja (wa makafiri), Tungejaalia wanaomkufuru Ar-Rahmaan wana nyumba zao zenye dari za fedha na ngazi pia wanazozipandia.[13] 

 

 

وَلِبُيُوتِهِمْ أَبْوَابًا وَسُرُرًا عَلَيْهَا يَتَّكِئُونَ﴿٣٤﴾

34. Na kwenye nyumba zao milango na makochi (ya fedha) wanayoyaegemea.

 

 

 

وَزُخْرُفًا ۚ وَإِن كُلُّ ذَٰلِكَ لَمَّا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَالْآخِرَةُ عِندَ رَبِّكَ لِلْمُتَّقِينَ﴿٣٥﴾

35. Na mapambo ya dhahabu. Lakini hayo yote si chochote isipokuwa ni starehe ya uhai wa dunia. Na Aakhirah iliyo kwa Rabb wako ni kwa wenye taqwa.

 

 

 

 

وَمَن يَعْشُ عَن ذِكْرِ الرَّحْمَـٰنِ نُقَيِّضْ لَهُ شَيْطَانًا فَهُوَ لَهُ قَرِينٌ﴿٣٦﴾

36. Na anayejifanya kipofu na ukumbusho wa Ar-Rahmaan Tunamwekea shaytwaan awe ndiye rafiki yake mwandani.

 

 

 

 

وَإِنَّهُمْ لَيَصُدُّونَهُمْ عَنِ السَّبِيلِ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُم مُّهْتَدُونَ﴿٣٧﴾

37. Na hakika wao (mashaytwaan) wanawazuia njia na wanadhania kwamba wao wamehidika.

 

 

 

 

 

 

حَتَّىٰ إِذَا جَاءَنَا قَالَ يَا لَيْتَ بَيْنِي وَبَيْنَكَ بُعْدَ الْمَشْرِقَيْنِ فَبِئْسَ الْقَرِينُ﴿٣٨﴾

38. Mpaka atakapotujia (Siku ya Qiyaamah), atasema: Laiti ingelikuwa baina yangu na baina yako umbali wa Mashariki na Magharibi, basi muovu mno rafiki mwandani wewe![14]

 

 

 

 

 

وَلَن يَنفَعَكُمُ الْيَوْمَ إِذ ظَّلَمْتُمْ أَنَّكُمْ فِي الْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ﴿٣٩﴾

39. Hakutokufaeni chochote leo nyinyi kuwa pamoja ndani ya adhabu, kwani mlidhulumu.

 

 

 

 

 

أَفَأَنتَ تُسْمِعُ الصُّمَّ أَوْ تَهْدِي الْعُمْيَ وَمَن كَانَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٤٠﴾

40. Je, kwani wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unaweza kusikilizisha viziwi au kuwahidi vipofu na yule aliye katika upotofu bayana?

 

 

 

 

 

فَإِمَّا نَذْهَبَنَّ بِكَ فَإِنَّا مِنْهُم مُّنتَقِمُونَ﴿٤١﴾

41. Na hata kama Tukikuondoa (kukufisha ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi hakika Sisi Ni Wenye Kuwalipizia.

 

 

 

 

 

أَوْ نُرِيَنَّكَ الَّذِي وَعَدْنَاهُمْ فَإِنَّا عَلَيْهِم مُّقْتَدِرُونَ﴿٤٢﴾

42. Au Tukuonyeshe yale Tuliyowatishia, basi hakika Sisi Ni Wenye Uwezo juu yao.

 

 

 

 

فَاسْتَمْسِكْ بِالَّذِي أُوحِيَ إِلَيْكَ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٤٣﴾

43. Basi shikilia kwa uthabiti yale uliyofunuliwa Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), hakika wewe uko juu ya njia iliyonyooka.

 

 

 

 

وَإِنَّهُ لَذِكْرٌ لَّكَ وَلِقَوْمِكَ ۖ وَسَوْفَ تُسْأَلُونَ﴿٤٤﴾

44. Na hakika hii (Qur-aan) bila shaka ni ukumbusho kwako na kwa watu wako, na mtakuja ulizwa.

 

 

 

 

وَاسْأَلْ مَنْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رُّسُلِنَا أَجَعَلْنَا مِن دُونِ الرَّحْمَـٰنِ آلِهَةً يُعْبَدُونَ﴿٤٥﴾

45. Na waulize (wafuasi wa) wale Tuliowatuma kabla yako miongoni mwa Rusuli Wetu: Je, Tulifanya badala ya Ar-Rahmaan waabudiwa wengine ili waabudiwe?

 

 

 

 

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَقَالَ إِنِّي رَسُولُ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴿٤٦﴾

46. Na kwa yakini Tulimtuma Muwsaa na Aayaat (Ishara, Dalili) Zetu kwa Firawni na wakuu wake akasema: (kuwaambia): Hakika mimi ni Rasuli wa Rabb wa walimwengu.

 

 

 

 

فَلَمَّا جَاءَهُم بِآيَاتِنَا إِذَا هُم مِّنْهَا يَضْحَكُونَ﴿٤٧﴾

47. Basi alipowajia na Aayaat (Ishara, Dalili) Zetu mara wao wakaharakia kuzicheka.

 

 

 

 

وَمَا نُرِيهِم مِّنْ آيَةٍ إِلَّا هِيَ أَكْبَرُ مِنْ أُخْتِهَا ۖ وَأَخَذْنَاهُم بِالْعَذَابِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ﴿٤٨﴾

48. Na Hatukuwaonyesha Aayah (Ishara, Dalili) yoyote isipokuwa ilikuwa ni kubwa zaidi kuliko ya mwenziwe, na Tukawachukua kwa adhabu ili wapate kurejea.

 

 

 

 

وَقَالُوا يَا أَيُّهَ السَّاحِرُ ادْعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَ إِنَّنَا لَمُهْتَدُونَ﴿٤٩﴾

49. Na wakasema: Ee mchawi! Tuombee kwa Rabb wako yale Aliyokuahidi kwako. Hakika sisi bila shaka tutaongoka.

 

 

 

 

 

فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُمُ الْعَذَابَ إِذَا هُمْ يَنكُثُونَ﴿٥٠﴾

50. Lakini Tulipowaondoshea adhabu, mara hao wanaharakia kuvunja ahadi.

 

 

 

 

وَنَادَىٰ فِرْعَوْنُ فِي قَوْمِهِ قَالَ يَا قَوْمِ أَلَيْسَ لِي مُلْكُ مِصْرَ وَهَـٰذِهِ الْأَنْهَارُ تَجْرِي مِن تَحْتِي ۖ أَفَلَا تُبْصِرُونَ﴿٥١﴾

51. Na Firawni akanadi kwa kaumu yake, akasema: Enyi kaumu yangu! Je, kwani ufalme wa Misri si wangu! Na hii mito inapita chini yangu? Je, hamuoni?

 

 

 

 

أَمْ أَنَا خَيْرٌ مِّنْ هَـٰذَا الَّذِي هُوَ مَهِينٌ وَلَا يَكَادُ يُبِينُ﴿٥٢﴾

52. Au mimi si bora kuliko huyu (Muwsaa) ambaye yeye ni dhalili na wala hawezi kujieleza wazi ila kwa mashaka?

 

 

 

 

 

فَلَوْلَا أُلْقِيَ عَلَيْهِ أَسْوِرَةٌ مِّن ذَهَبٍ أَوْ جَاءَ مَعَهُ الْمَلَائِكَةُ مُقْتَرِنِينَ﴿٥٣﴾

53. Basi kwa nini hakuvishwa vikuku vya dhahabu, au wakaja pamoja naye Malaika wenye kuandamana naye?

 

 

 

 

 

فَاسْتَخَفَّ قَوْمَهُ فَأَطَاعُوهُ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ﴿٥٤﴾

54. Basi aliwachezea akili watu wake nao wakamtii. Hakika wao walikuwa watu mafasiki.

 

 

 

 

فَلَمَّا آسَفُونَا انتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَأَغْرَقْنَاهُمْ أَجْمَعِينَ﴿٥٥﴾

55. Basi walipotukasirisha, Tuliwalipizia, Tukawagharikisha wote.

 

 

 

 

 

فَجَعَلْنَاهُمْ سَلَفًا وَمَثَلًا لِّلْآخِرِينَ﴿٥٦﴾

56. Tukawafanya wenye kutangulia na mfano kwa wengineo.

 

 

 

 

وَلَمَّا ضُرِبَ ابْنُ مَرْيَمَ مَثَلًا إِذَا قَوْمُكَ مِنْهُ يَصِدُّونَ﴿٥٧﴾

57. Na mwana wa Maryam aliponukuliwa kama mfano, tahamaki watu wako wanaupigia kelele na kushangilia.[15]

 

 

 

وَقَالُوا أَآلِهَتُنَا خَيْرٌ أَمْ هُوَ ۚ مَا ضَرَبُوهُ لَكَ إِلَّا جَدَلًا ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ خَصِمُونَ﴿٥٨﴾

58. Na wakasema: Je, waabudiwa wetu ni bora au yeye? Hawakukupigia (mfano) huo isipokuwa tu kutaka ubishi. Bali wao ni watu makhasimu.

 

 

 

 

إِنْ هُوَ إِلَّا عَبْدٌ أَنْعَمْنَا عَلَيْهِ وَجَعَلْنَاهُ مَثَلًا لِّبَنِي إِسْرَائِيلَ﴿٥٩﴾

59. Yeye (Nabiy ‘Iysaa) si chochote isipokuwa ni mja Tuliyemneemesha, na Tukamfanya ni mfano kwa wana wa Israaiyl.

 

 

 

 

وَلَوْ نَشَاءُ لَجَعَلْنَا مِنكُم مَّلَائِكَةً فِي الْأَرْضِ يَخْلُفُونَ﴿٦٠﴾

60. Na lau Tungelitaka, basi Tungewafanya Malaika badala yenu wanarithishana katika ardhi.

 

 

 

 

وَإِنَّهُ لَعِلْمٌ لِّلسَّاعَةِ فَلَا تَمْتَرُنَّ بِهَا وَاتَّبِعُونِ ۚ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ﴿٦١﴾

61. Na hakika yeye (Nabiy ‘Iysaa) ni alama ya Saa.[16] Basi musiitilie shaka, na nifuateni. Hii ndio njia iliyonyooka.

 

 

 

 

وَلَا يَصُدَّنَّكُمُ الشَّيْطَانُ ۖ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ﴿٦٢﴾

62. Na jitahidini sana asikuzuieni shaytwaan, hakika yeye kwenu ni adui bayana.

 

 

 

 

وَلَمَّا جَاءَ عِيسَىٰ بِالْبَيِّنَاتِ قَالَ قَدْ جِئْتُكُم بِالْحِكْمَةِ وَلِأُبَيِّنَ لَكُم بَعْضَ الَّذِي تَخْتَلِفُونَ فِيهِ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ﴿٦٣﴾

63. Na alipokuja ‘Iysaa kwa hoja bayana, akasema: Nimekujieni na hikmah, na ili nikubainishieni baadhi ya yale mnayokhitilafiana kwayo, basi mcheni Allaah na nitiini.

 

 

 

 

إِنَّ اللَّـهَ هُوَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ﴿٦٤﴾

64. Hakika Allaah Ndiye Rabb wangu na Rabb wenu, basi mwabuduni Yeye Pekee,[17] hii ndio njia iliyonyooka.

 

 

 

 

فَاخْتَلَفَ الْأَحْزَابُ مِن بَيْنِهِمْ ۖ فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْ عَذَابِ يَوْمٍ أَلِيمٍ﴿٦٥﴾

65. Basi wakakhitilafiana makundi kwa makundi baina yao.[18] Basi ole kwa wale waliodhulumu kutokana na adhabu ya Siku iumizayo.

 

 

 

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا السَّاعَةَ أَن تَأْتِيَهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ﴿٦٦﴾

66. Je, wanangojea isipokuwa Saa tu iwafikie ghafla nao hawatambui.

 

 

 

 

الْأَخِلَّاءُ يَوْمَئِذٍ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ إِلَّا الْمُتَّقِينَ﴿٦٧﴾

67. Marafiki wapenzi Siku hiyo watakuwa maadui wao kwa wao isipokuwa wenye taqwa.

 

 

 

يَا عِبَادِ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمُ الْيَوْمَ وَلَا أَنتُمْ تَحْزَنُونَ﴿٦٨﴾

68. Enyi Waja Wangu! Hakuna khofu juu yenu leo, na wala nyinyi hamtohuzunika.

 

 

 

 

الَّذِينَ آمَنُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا مُسْلِمِينَ﴿٦٩﴾

69. Ambao wameamini Aayaat (na Ishara, Dalili) Zetu na wakawa Waislamu.

 

 

 

ادْخُلُوا الْجَنَّةَ أَنتُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ تُحْبَرُونَ﴿٧٠﴾

70. Ingieni Jannah nyinyi na wake zenu mfurahishwe.

 

 

 

 

يُطَافُ عَلَيْهِم بِصِحَافٍ مِّن ذَهَبٍ وَأَكْوَابٍ ۖ وَفِيهَا مَا تَشْتَهِيهِ الْأَنفُسُ وَتَلَذُّ الْأَعْيُنُ ۖ وَأَنتُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴿٧١﴾

71. Watapitishiwa sahani za dhahabu na bilauri. Na humo mna yale zinazotamani nafsi na ya kuburudisha macho, nanyi humo ni wenye kudumu.

 

 

 

 

وَتِلْكَ الْجَنَّةُ الَّتِي أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٧٢﴾

72. Na hiyo ni Jannah ambayo mmerithishwa kwa yale mliyokuwa mkitenda.

 

 

 

 

لَكُمْ فِيهَا فَاكِهَةٌ كَثِيرَةٌ مِّنْهَا تَأْكُلُونَ﴿٧٣﴾

73. Mtapata humo matunda mengi, mtakula yoyote myatakayo.

 

 

 

 

إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي عَذَابِ جَهَنَّمَ خَالِدُونَ﴿٧٤﴾

74. Hakika wahalifu watadumu kwenye adhabu ya Jahannam.

 

 

 

 

لَا يُفَتَّرُ عَنْهُمْ وَهُمْ فِيهِ مُبْلِسُونَ﴿٧٥﴾

75. Hawatopumzishwa nayo, nao humo watakata tamaa.

 

 

 

 

وَمَا ظَلَمْنَاهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا هُمُ الظَّالِمِينَ﴿٧٦﴾

76. Na wala Hatukuwadhulumu, lakini walikuwa wao wenyewe ndio madhalimu.

 

 

 

 

وَنَادَوْا يَا مَالِكُ لِيَقْضِ عَلَيْنَا رَبُّكَ ۖ قَالَ إِنَّكُم مَّاكِثُونَ﴿٧٧﴾

77. Na wataita: Ee Maalik![19] Na Atumalize tufe Rabb wako. Atasema: Hakika nyinyi ni wenye kubakia kuishi humo.

 

 

 

 

لَقَدْ جِئْنَاكُم بِالْحَقِّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَكُمْ لِلْحَقِّ كَارِهُونَ﴿٧٨﴾

78. Kwa yakini Tulikujieni na haki, lakini wengi wenu ni wenye kuichukia haki.

 

 

 

أَمْ أَبْرَمُوا أَمْرًا فَإِنَّا مُبْرِمُونَ﴿٧٩﴾

79. Au je walipanga njama zao barabara?  Basi hakika Sisi Ni Wenye Kulipiza njama.

 

 

 

 

أَمْ يَحْسَبُونَ أَنَّا لَا نَسْمَعُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَاهُم ۚ بَلَىٰ وَرُسُلُنَا لَدَيْهِمْ يَكْتُبُونَ﴿٨٠﴾

80. Au wanadhania kwamba Sisi Hatusikii siri zao na minong’ono yao? Bali ndio (Tunasikia!) Na Wajumbe Wetu wako kwao wanaandika.

 

 

 

 

قُلْ إِن كَانَ لِلرَّحْمَـٰنِ وَلَدٌ فَأَنَا أَوَّلُ الْعَابِدِينَ﴿٨١﴾

81. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Kama ingelikuwa Ar-Rahmaan Ana mwana (kama mnavyodai), basi mimi ningekuwa wa mwanzo katika waja (Wake).[20]

 

 

 

 

سُبْحَانَ رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبِّ الْعَرْشِ عَمَّا يَصِفُونَ﴿٨٢﴾

82. Utakasifu ni wa Rabb wa mbingu na ardhi, Rabb wa ‘Arsh kutokana na yale wanayoyavumisha. 

 

 

 

 

فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّىٰ يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ﴿٨٣﴾

83. Basi waachilie mbali watumbukie katika porojo na wacheze mpaka wakutane na Siku yao wanayoahidiwa.

 

 

 

 

وَهُوَ الَّذِي فِي السَّمَاءِ إِلَـٰهٌ وَفِي الْأَرْضِ إِلَـٰهٌ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ﴿٨٤﴾

84. Na Yeye Ndiye Muabudiwa wa haki mbinguni na ardhini pia (Ndiye Huyo Huyo) Ilaah. Naye Ndiye Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.[21]

 

 

وَتَبَارَكَ الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَعِندَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴿٨٥﴾

85. Na Amebarikika Ambaye ufalme wa mbingu na ardhi ni Wake na vilivyo baina yake, na Kwake Pekee upo ujuzi wa Saa, na Kwake mtarejeshwa.

 

 

 

 

وَلَا يَمْلِكُ الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ الشَّفَاعَةَ إِلَّا مَن شَهِدَ بِالْحَقِّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ﴿٨٦﴾

86. Na wala wale wanaowaomba badala Yake hawana uwezo wa kumiliki uombezi isipokuwa yule aliyeshuhudia kwa haki nao wanajua.[22]

 

 

 

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَهُمْ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ﴿٨٧﴾

87. Na ukiwauliza: Ni nani kawaumba? Bila shaka watasema: Allaah.  Basi vipi wanaghilibiwa?[23]

 

 

 

 

وَقِيلِهِ يَا رَبِّ إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ قَوْمٌ لَّا يُؤْمِنُونَ﴿٨٨﴾

88. Na (Allaah Anajua) kauli yake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Ee Rabb wangu!  Hakika hawa watu hawaamini.

 

 

 

 

فَاصْفَحْ عَنْهُمْ وَقُلْ سَلَامٌ ۚ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ﴿٨٩﴾

89. Basi wapuuzilie mbali (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na sema: Salaamun! Na karibuni hivi watakuja jua.

 

 

 

 

 

 

 

 

[1] الحروف المقطعة  (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):

 

Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة  (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).

 

[2] Ummul-Kitaab: Mama Wa Kitabu Ni Lawh Mahfudhw (Ubao Uliohifadhiwa) Rejea: Ar-Ra’d (13:39).

 

[3]  Washirikina Kuipuuza Qur-aan:

 

‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu Aayah hii kama ifuatavyo:

 

Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما), Abu Swalih, Mujaahid na As-Suddi na ni rai ya Ibn Jariyr pia: “Mnadhani Tutakusameheni na Hatutakuadhibuni, na hali hamfanyi mliyoamrishwa?”

 

Qataadah: “Naapa kwa Allaah, lau kuwa Qur-aan hii ingeondolewa walipoikataa vizazi vya mwanzo vya Ummah huu, wangeliangamia, lakini Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Rehma Yake Amerudia kuituma kama Desturi Yake na kuwalingania kwa muda wa miaka ishirini, au kwa muda mrefu kama Alivyotaka.”

 

Tafsiyr ya Imaam As-Sa’diy (رحمه الله):

 

Hivi Tuwapuuze na Tuache kuteremsha ukumbusho, na Tuwaondoshelee mbali Ukumbusho kwa ajili ya kupuuza kwenu? Bali Tunawateremshia Kitabu na Tunaweka wazi kwenu kila kitu, na kama mtaamini na mkaongoka, basi hilo ni katika tawfiyq yenu, na kama si hivyo, basi itasimama hoja juu yenu na mtakuwa kwenye ubainisho wa jambo lenu. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

[4] Washirikina Waliamini Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah Lakini Walikanusha Tawhiyd Al-Uluwhiyyah::

 

Rejea Yuwnus (10:31), Al-‘Ankabuwt (29:61).

 

[5] Mfano Wa Ardhi Iliyokufa (Kame), Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akaihuisha Kwa Mvua, Ni Mfano Wa Kuwahuisha Watu Kutoka Makaburini Mwao Siku Ya Qiyaamah:

 

Rejea Ar-Ruwm (30:50).

 

[6] Duaa Ya Kupanda Kipando:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho kwenye duaa ya kupanda chombo:

 

095-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kupanda Mnyama Au Chombo Chochote Cha Kusafiria

 

Na Hadiyth yake ni ifuatayo:

 

عن عَلِي بن ربيعة ، قَالَ : شهدت عليَّ بن أَبي طالب رضي الله عنه ، أُتِيَ بِدَابَّةٍ لِيَرْكَبَهَا ، فَلَمَّا وَضَعَ رِجْلَهُ في الرِّكَابِ ، قَالَ : بِسْمِ اللهِ ، فَلَمَّا اسْتَوَى عَلَى ظَهْرِهَا ، قَالَ : الحَمْدُ للهِ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنينَ ، وَإنَّا إِلَى رَبِّنَا لَمُنْقَلِبُونَ ، ثُمَّ قَالَ : الحمْدُ للهِ ، ثَلاثَ مَرَّاتٍ ، ثُمَّ قَالَ : اللهُ أكْبَرُ ، ثَلاثَ مَرَّاتٍ ، ثُمَّ قَالَ : سُبْحَانَكَ إنّي ظَلَمْتُ نَفْسِي فَاغْفِرْ لِي إنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أنْتَ ، ثُمَّ ضَحِكَ ، فَقيلَ : يَا أمِيرَ المُؤمِنِينَ ، مِنْ أيِّ شَيْءٍ ضَحِكْتَ ؟ قَالَ : رَأيتُ النبيَّ صلى الله عليه وسلم فَعَلَ كَمَا فَعَلْتُ ثُمَّ ضَحِكَ ، فقُلْتُ : يَا رسول اللهِ ، مِنْ أيِّ شَيْءٍ ضَحِكْتَ ؟ قَالَ : ((  إنَّ رَبَّكَ تَعَالَى يَعْجَبُ مِنْ عَبدِهِ إِذَا قَالَ : اغْفِرْ لِي ذُنُوبِي ، يَعْلَمُ أنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ غَيْرِي )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن ))، وفي بعض النسخ: (( حسن صحيح )) . وهذا لفظ أَبي داود .

 

 'Aliy bin Rabiy’ah (رضي الله عنه)  amesema: Nimemshuhudia 'Aliy bin Abiy Twaalib (رضي الله عنه)  akiletewa mnyama ampande. Alipoweka mguu wake kwenye kipando alisema:

 

بِسْمِ اللهِ

Alipolingana juu ya mgongo wake alisema:

 

  الحَمْدُ للهِ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنينَ ، وَإنَّا إِلَى رَبِّنَا لَمُنْقَلِبُونَ    

Kisha akasema:

 الحمْدُ للهِ

 

AlhamduliLlaah (Himdi Anastahiki Allaah) (mara tatu).

 

Kisha akasema:

اللهُ أكْبَرُ
 

Allaahu Akbar (Allaah Ni Mkubwa) (mara tatu).

 

Kisha akasema:

 

  سُبْحَانَكَ إنّي ظَلَمْتُ نَفْسِي فَاغْفِرْ لِي إنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أنْتَ

Subhaanak inniy dhwalamtu nafsiy Faghfirliy, innahu laa yaghfirudh-dhunuwba illa Anta.

 

Kutakasika ni Kwako, hakika mimi nimedhulumu nafsi yangu, basi Nighufurie, kwani hakuna mwenye kughufuria dhambi ila Wewe. 

 

Kisha akacheka. Akaulizwa: Ee Amiri wa Waumini! Unacheka nini?

 

Akasema: Nilimuona Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akifanya kama nilivyofanya, kisha akacheka. Nikamuuliza: Ee Rasuli wa Allaah! Unacheka nini? Akasema: “Hakika Rabb wako Anamridhia mja Wake anaposema: Nighufurie dhambi zangu, anajua kuwa hakuna anayeghufuria dhambi isipokuwa Mimi.”

 

[Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy, amesema ni Hadiyth Hasan. Na katika baadhi ya mapokezi ni Hadiyth Hasan Swahiyh, na hii ni lafdhi ya Abuu Daawuwd]

 

Rejea Suwrah Nuwh (11:41), Al-Muuminuwn (23:28-28).

 

[7] Washirikina Kumsingizia Allaah Ana Wana:

 

Rejea An-Nisaa (4:191), Al-Maaidah (5:17), At-Tawbah (9:30), Asw-Swaaffaat (37:149) (37:158).

 

[8] Wamemzulia Allaah (سبحانه وتعالى) Ana Wana Wa Kike:

 

Rejea Asw-Swaaffaat: (37:149), Al-Israa (17:40), An-Nahl (57-59).

 

[9] Wao Wenyewe Wanawachukia Wana Wa Kike Lakini Wanawahusisha Na Allaah (عزّ وجلّ): Rejea An-Nahl: (16:57-59), Asw-Swaaffaat (37:149) (37:158).

 

[10] Washirikina Kumsingizia Allaah Ana Wana Na Kwamba Ni Wana Wa Kike:

 

Rejea Suwrah hii Az-Zukhruf (43:15) hadi Aayah hii ya (19), na faida zake.

 

Rejea pia An-Nisaa (4:191), Al-Maaidah (5:17), At-Tawbah (9:30), Asw-Swaaffaat (37:149) (37:158). Al-Israa (17:40), An-Nahl (57-59).

 

[11] Kufuata Mababa Na Mababu Japokuwa Hawakuwa Na Ilimu Na Walikuwa Wapotofu:

 

Aayah hii na ifuatayo inataja ujahili wa watu kufuata kibubusa upotofu wa baba na babu zao, japokuwa hawakuwa na ilimu. 

 

Rejea pia Aayah zifuatazo zinazothibitisha hayo pia:

 

Al-Baqarah (2:170),  Al-Maaidah (5:104), Al-A’raaf (7:28), (7:65-71), Yuwnus (10:75-78), Al-Anbiyaa (21:52-53), Ash-Shu’araa (26:69-76), Luqmaan (31:21).

 

Hali hiyo ni sawa na hali ya baadhi ya watu wa ummah huu wanaofuata mambo yasiyokuwemo katika Dini, bali ni vile kufuata yale ya shirki na bid’ah yaliyokuwa yakizoeleka kutendwa na watu wao waliotangulia.

 

[12] Mtu Mtukufu Na Miji Miwili:

 

Washirikina walidai kwa nini Qur-aan isiteremshwe kwa mtu mtukufu kama Waliyd Bin Mughiyrah au Mas’uwd bin ‘Amru Ath-Thaqafiyy, au ‘Utbah bin Rabiy’ au Habiyb bin ‘Amru. 

 

Miji miwili ni Makkah na Twaaif. [Tafsiyr Ibn Kathiyr, As-Sa’diy, Tafsiyr Al-Muyassar]

 

[13] Allaah (سبحانه وتعالى) Kutokuwapanulia Waja Wake Mali, Mapambo Na Starehe Za Dunia Kwa Ajili Ya Kutokuingia Katika Kufru Na Maasi:

 

Tafsiyr ya Aayah zifuatazo (33-35):

 

وَلَوْلَا أَن يَكُونَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً لَّجَعَلْنَا لِمَن يَكْفُرُ بِالرَّحْمَـٰنِ لِبُيُوتِهِمْ سُقُفًا مِّن فِضَّةٍ وَمَعَارِجَ عَلَيْهَا يَظْهَرُونَ﴿٣٣﴾

Na lau isingelikuwa watu watakuwa ummah mmoja (wa makafiri), Tungejaalia wanaomkufuru Ar-Rahmaan wana nyumba zao zenye dari za fedha na ngazi pia wanazozipandia.

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Anakhabarisha kwamba dunia haiwi sawa na chochote Kwake, na kwamba kama si Upole na Huruma Yake kwa Waja Wake ambayo haitanguliwi na chochote, basi Angeikunjua dunia kwa wale waliokufuru, na Angejaalia ngazi za fedha wanazipanda.  

وَلِبُيُوتِهِمْ أَبْوَابًا وَسُرُرًا عَلَيْهَا يَتَّكِئُونَ﴿٣٤﴾

 

Na kwenye nyumba zao milango na makochi (ya fedha) wanayoyaegemea.

 

Na Angewajaalia wao mapambo ya dunia kila aina, na Angewapa vile wanavyovitamani. Lakini kilichozuia ni Huruma Yake kwa Waja Wake kwa kuogopea watu wasije kuharakisha kuingia katika ukafiri na kufanya maasi kwa wingi kwa sababu ya kuipenda dunia.

 

وَزُخْرُفًا ۚ وَإِن كُلُّ ذَٰلِكَ لَمَّا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَالْآخِرَةُ عِندَ رَبِّكَ لِلْمُتَّقِينَ﴿٣٥﴾

Na mapambo ya dhahabu. Lakini hayo yote si chochote isipokuwa ni starehe ya uhai wa dunia. Na Aakhirah iliyo kwa Rabb wako ni kwa wenye taqwa.

 

Katika maelezo haya, kuna dalili ya kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Anawanyima Waja Wake baadhi ya mambo ya kidunia kwa kuwazuia kabisa au uzuiaji khaswa (vitu maalum), kwa ajili ya maslahi yao, na kwamba dunia haifanani mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى) japo na ubawa wa mbu, na kwamba hivi vilivyotajwa vyote ni starehe ya kidunia tu yenye malengo yasiyotimia, yaliyotibuka na yenye kwisha. Ama Aakhirah mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى) ni bora kwa wanaomcha Allaah, kwa kufuata Amri Zake na kujiepusha na Makatazo Yake, kwani Neema Zake zimetimia na kukamilika kila upande, na katika Jannah (Pepo) kuna yanayotamaniwa na nafsi na yenye kuburudisha macho, wataishi humo milele. Basi utofauti ulioje kati ya makazi haya mawili! [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

[14] Shaytwaan Huwapotosha Watu Kisha Huwakanusha Na Kuwageuka!:

 

Rejea Ibraahiym (14:22) kwenye maelezo na rejea mbalimbali.

 

[15]  Makafiri Kushangilia Kauli Ya Allaah (سبحانه وتعالى)  Waliyoifahamu Ndivyo Sivyo:

 

Na Sababu Ya Kuteremshwa Aayah:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho chenye Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah au Suwrah:

 

043-Asbaabun-Nuzuwl: Az-Zukhruf Aayah 57: وَلَمَّا ضُرِبَ ابْنُ مَرْيَمَ مَثَلا إِذَا قَوْمُكَ مِنْهُ يَصِدُّونَ

 

Na washirikina walipopiga mfano wa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام)  mwana wa Maryam, walipomjadili Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumhoji kuwa Manaswara wanamuabudu, unawakuta watu wako wanainua sauti zao na kupiga kelele kwa furaha na kuterema. Napo ni pale Kauli ya Allaah (عزّ وجلّ) ilipoteremka:

 

إِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ حَصَبُ جَهَنَّمَ أَنتُمْ لَهَا وَارِدُونَ ﴿٩٨﴾

Hakika nyinyi na yale mnayoyaabudu badala ya Allaah ni vichochezi vya moto wa Jahannam, nyinyi mtauingia. [Al-Anbiyaa (21:98)]

 

Bonyeza kiungo kifuatacho kwenye maelezo bayana na Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah.

 

021-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Anbiyaa Aayah 101: إِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ حَصَبُ جَهَنَّمَ أَنتُمْ لَهَا وَارِدُونَ

 

Na washirikina wakasema: Tumeridhika kwa waabudiwa (masanamu) wetu wawe na cheo cha ‘Iysaa.” Basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:

 

إِنَّ الَّذِينَ سَبَقَتْ لَهُم مِّنَّا الْحُسْنَىٰ أُولَـٰئِكَ عَنْهَا مُبْعَدُونَ ﴿١٠١﴾

Hakika wale ambao imewatangulia Al-Husnaa (furaha, Rehma) kutoka Kwetu, hao watabaidishwa nao (moto). [Al-Anbiyaa (21:101]

 

[Tafsiyr Al-Muyassar]

 

Basi yule anayetupwa motoni, miongoni mwa waabudiwa wa makafiri, ni yule aliyeridhika kuabudiwa na wao. [Tafsiyr Al-Muyassar]

 

[16] Kuteremka Kwa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) Ni Katika Alama Kuu Za Qiyaamah.

 

Rejea Al-An’aam (6:158), An-Nisaa (4:159).

 

[17] Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) Anakiri Kuwa Yeye Ni Mja Wa Allaah Na Wala Sio Mwana Au Mshirika Wa Allaah.

 

Rejea Suwrah Maryam (19:30-36), Al-Maaidah (5:17), (5:72-76), (5:116-118), An-Nisaa (4:171).

 

[18] Makundi Kukhitilafiana Kuhusu Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام):

Hapo makundi ya watu yakatafautiana kuhusu jambo la ‘Iysaa (عليه السّلام) na wakawa mapote. Kati yao kuna waliokubali kuwa yeye ni mja wa Allaah na ni Rasuli Wake. Na hiyo ndio kauli ya kweli. Na kati yao kuna wanaodai kuwa yeye ni mwana wa Allaah. Na kati yao kuna wanaosema kwamba yeye ni Allaah! Ametukuka Allaah (سبحانه وتعالى) kutukuka kukubwa na kutakasika na neno lao hilo. Basi maangamivu na adhabu kali Siku ya Qiyaamah ni yenye kuwapata wale waliomwelezea Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) kwa sifa ambazo sizo zile Allaah (سبحانه وتعالى) Alizomsifu nazo. [Tafsiyr Al-Muyassar]

 

[19] Maalik: Ni Malaika Mlinzi Wa Moto.

 

Kuamini Malaika wa Allaah (سبحانه وتعالى) ni katika nguzo mojawapo ya nguzo sita za imaan.

 

Na Malaika wa Allaah (سبحانه وتعالى) ni wengi mno wala haijulikani idadi yao isipokuwa na Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee, na wala hakuna faida kujua idadi yao, bali Muislamu amewajibika kuamini kuwepo kwao tu.  Na kauli za Salaf kuhusu wingi wao ni kama zifuatavyo:

 

Kauli za ‘Ulamaa kuhusu wingi wa Malaika:   

 

Imaam Ibn Kathiyr (رحمه الله):  Hakuna anayejua idadi yao au wingi wao isipokuwa Yeye Allaah (سبحانه وتعالى). [Tafsiyr Ibn Kathiyr (8/270)]

 

Imaam An-Nawawiy (رحمه الله): Kuhusu Malaika wanaozunguka Bayt Al-Ma’muwr, rejea Hadiyth iliyotajwa katika namba (xvi).  

 

“Hii ni dalili kubwa kuhusu wingi wa Malaika (عليهم السّلام) na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi. [Sharh Muslim (2/225)]

 

Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah (رحمه الله): “Hakuna anayeweza kuhesabu idadi ya Malaika isipokuwa Allaah.” [Majmuw’ Al-Fataawaa (4/119)]

 

Malaika Wa Allaah Na Majukumu Yao:

 

Juu ya kuwa Malaika wa Allaah (سبحانه وتعالى) ni wengi mno, ila hatukujulishwa majina yao isipokuwa wafuatao kama ilivyothibiti katika Qur-aan na Sunnah:

 

(1) Jibriyl: Kuteremsha Wahyi. Rejea Ash-Shu’araa (26:193-194). Huyu ni Malaika mkuu kabisa kati ya Malaika wa Allaah (سبحانه وتعالى). 

 

 

(2) Maalik: Mlinzi wa moto. Aayah ya Suwrah hii Az-Zukhruf (42:77).

 

 

(3) Miykaaiyl:  Kuteremsha mvua. Rejea Al-Baqarah (2:98)

 

 

(4) Israafiyl:  Kupuliza baragumu Siku ya Qiyaamah. Rejea Al-Baqarah (2:98) kwenye Hadiyth iliyothibiti kutajwa kwake.

 

 

(5) Munkar na Nakiyr: 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ إِذَا قُبِرَ الْمَيِّتُ - أَوْ قَالَ أَحَدُكُمْ أَتَاهُ مَلَكَانِ أَسْوَدَانِ أَزْرَقَانِ يُقَالُ لأَحَدِهِمَا الْمُنْكَرُ وَالآخَرُ النَّكِيرُ فَيَقُولاَنِ مَا كُنْتَ تَقُولُ فِي هَذَا الرَّجُلِ فَيَقُولُ مَا كَانَ يَقُولُ هُوَ عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ ‏.‏ فَيَقُولاَنِ قَدْ كُنَّا نَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُولُ هَذَا ‏.‏ ثُمَّ يُفْسَحُ لَهُ فِي قَبْرِهِ سَبْعُونَ ذِرَاعًا فِي سَبْعِينَ ثُمَّ يُنَوَّرُ لَهُ فِيهِ ثُمَّ يُقَالُ لَهُ نَمْ ‏.‏ فَيَقُولُ أَرْجِعُ إِلَى أَهْلِي فَأُخْبِرُهُمْ فَيَقُولاَنِ نَمْ كَنَوْمَةِ الْعَرُوسِ الَّذِي لاَ يُوقِظُهُ إِلاَّ أَحَبُّ أَهْلِهِ إِلَيْهِ ‏.‏ حَتَّى يَبْعَثَهُ اللَّهُ مِنْ مَضْجَعِهِ ذَلِكَ ‏.‏ وَإِنْ كَانَ مُنَافِقًا قَالَ سَمِعْتُ النَّاسَ يَقُولُونَ فَقُلْتُ مِثْلَهُ لاَ أَدْرِي ‏.‏ فَيَقُولاَنِ قَدْ كُنَّا نَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُولُ ذَلِكَ ‏.‏ فَيُقَالُ لِلأَرْضِ الْتَئِمِي عَلَيْهِ ‏.‏ فَتَلْتَئِمُ عَلَيْهِ ‏.‏ فَتَخْتَلِفُ فِيهَا أَضْلاَعُهُ فَلاَ يَزَالُ فِيهَا مُعَذَّبًا حَتَّى يَبْعَثَهُ اللَّهُ مِنْ مَضْجَعِهِ ذَلِكَ ‏"‏ ‏.‏ وَفِي الْبَابِ عَنْ عَلِيٍّ وَزَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ وَابْنِ عَبَّاسٍ وَالْبَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ وَأَبِي أَيُّوبَ وَأَنَسٍ وَجَابِرٍ وَعَائِشَةَ وَأَبِي سَعِيدٍ كُلُّهُمْ رَوَوْا عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فِي عَذَابِ الْقَبْرِ ‏.وقَالَ أَبو عِيسَى : حديثٌ حَسَنٌ غَرِيب وحسنه في "صحيح الجامع" رقم : (724).

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Anapozikwa maiti”  au amesema: “Mmoja wenu anapozikwa, Malaika wawili weusi wenye macho kibuluu watamjia. Mmoja wao anaitwa Al-Munkar na mwingine anaitwa Al-Nakiyr, watamuuliza: Ulikuwa ukisema nini kuhusu mtu huyu? (Maiti) atasema yale aliyokuwa akisema (duniani): Yeye ni mja wa Allaah na Rasuli Wake na

 

أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ

 

Ninashuhudia kwamba hakuna mwabudiwa wa haki ila Allaah na kwamba Muhammad ni Mja Wake na Rasuli Wake.

 

Basi watasema: Hakika tulikuwa tunajua kuwa utasema haya. Kisha kaburi lake litapanuliwa hadi dhiraa sabini kwa sabini, kisha litajazwa nuru kwa ajili yake na ataambiwa: Lala! Atasema: Je naweza kurudi kwa ahli zangu na kuwajulisha? Watasema: Lala kama usingizi wa mwana arusi mpya hakuna anayemwamsha isipokuwa aliyekuwa ni mpendwa zaidi wa familia yake.  (Atalala) mpaka Allaah Atakapomfufua kutoka mahali pake hapo  pa kupumzika. Na ikiwa ni mnafiki atasema: Mimi nilikuwa nasikia watu wakisema hivyo nami nikasema sawa na wasemavyo, sijui! Watasema: Tulijua kwamba utasema hivyo!  Kisha ardhi itaambiwa: Mbane! Basi ardhi itambana hadi mbavu zake zipishane, ataendelea kuadhibiwa hivyo hadi Allaah Atakampofufua kutoka mahali pake hapo pa kupumzika.” [At-Tirmidhiy, na Abuu ‘Iysaa amesema: Hadiyth Hasan Ghariyb, na ameipa daraja ya Hasan katika Swahiyh Al-Jaami’ (724)]      

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Anapozikwa maiti”  au amesema: “Mmoja wenu anapozikwa, Malaika wawili weusi na buluu watamjia. Mmoja wao   anaitwa Al-Munkar na mwingine anaitwa Al-Nakiyr watasema: Mlikuwa mkisema nini kuhusu mtu huyu? Hivyo  mtu huyo atasema yale aliyokuwa akisema (duniani): Yeye ni mja wa Allaah na Rasuli Wake na

 

أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ

Ninashuhudia kwamba hakuna mwabudiwa wa haki ila Allaah na kwamba Muhammad ni Mja Wake na Rasuli Wake.

 

Basi watasema: Hakika tulikuwa tunajua kuwa utasema haya. Kisha kaburi lake linapanuliwa hadi dhiraa sabini kwa sabini, kisha litamulikwa kwa ajili yake na ataambiwa : Lala! Atasema: Je naweza kurudi kwa ahli zangu na kuwajulisha?  Watasema: Lala  kama usingizi wa mwana arusi mpya hakuna anayemwamsha isipokuwa aliyekuwa ni mpendwa zaidi wa familia yake.  (Atalala) mpaka Allaah Atamfufua kutoka mahali pale pa kupumzika. Na ikiwa ni mnafiki atasema: Mimi nilisika watu wakisema hivyo nami nikasema sawa na wasemavyo: Sijui!  Watasema: Tulijua kwamba utasema hivyo!  Kisha ardhi itaambiwa: Mbane! Basi ardhi itambana na itambana mbavu zake, ataendelea kuadhibiwa hivyo hadi Allaah Atakampofufua kutoka mahali pake hapo pa kupmzika.” [At-Tirmidhiy, na Abuu ‘Iysaa amesema: Hadiyth Hasan Ghariyb, na ameipa daraja ya Hasan katika Swahiyh Al-Jaami’ (724)]       

 

 

(6) Haaruwt na Maaruwt: Malaika wawili ambao Allaah (عزّ وجلّ) Aliwateremsha ardhini kuwa ni fitnah (jaribio na mtihani) kwa watu ili wawafundishe sihri (uchawi). Rejea Al-Baqarah (2:102).  

 

Na wafuatao ni Malaika wachache wengineo ambao hawakutajwa majina yao, ila yametajwa majukumu yao na kazi zao, nao ni kama ifuatavyo:

 

 

(7) Wenye kazi ya kutoa roho za watu. Huyu ametajwa kama Malakul-Mawt (Malaika anayetoa roho). Rejea Al-An’aam (6:61), As-Sajdah (32:11), .

 

 

(8) Wanaowahifadhi na kuwalinda wanaadam wasipatwe na madhara yoyote katika harakaat zao mchana na usiku. Rejea Al-An’aam (6:61), na wako wenye kuhifadhi wanaadam kwa zamu katika jukumu hili. Rejea Ar-Ra’d (13:10-11).

 

 

(9) Walinzi wa milango ya Jannah. Rejea Az-Zumar (39:73), Ar-Ra’d (13:23-24).

 

 

(10) Walinzi wa moto wa Jahannam.

 

Rejea Az-Zumar (39:71), Al-Muddath-thir (74:30-31) ambako imetajwa idadi yao kuwa ni kumi na tisa. Pia rejea Al-‘Alaq (96:18), Al-Mulk (67:8). Na Hadiyth ifuatayo imetaja idadi ya Malaika 4,900,000,000 (70,000 X 70,000) kuhusiana na moto wa Jahannam:  

 

عن ابن مسعود رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( يُؤتَى بِجَهَنَّمَ يَومَئذٍ لَهَا سَبْعُونَ ألفَ زِمَامٍ ، مَعَ كُلِّ زِمَامٍ سَبعُونَ ألْفَ مَلَكٍ يَجُرُّونَهَا )) رواه مسلم .

Amesimulia Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Siku hiyo ya Qiyaamah Jahannam italetwa ikiwa na hatamu elfu sabiini pamoja na kila hatamu kutakuwa na Malaika elfu sabiini  wanaoikokota." [Muslim]

 

 

(11) Wenye kuhifadhi na kuandika mema na shari wanazotenda wanaadam. Rejea Suwrah hii Az-Zukhruf (43:80), Al-An’aam (6:61), Qaaf (50:17-18), Al-Infitwaar (82:11).

 

 

(12) Wenye kubeba ‘Arsh ya Allaah. Rejea Ghaafir (7:7), Al-Haaqqah (69:17).

 

(xiii) Wenye kuandika majaaliwa ya mwanaadam pindi mimba inapofika miezi minne katika tumbo la mama kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:

 

عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم -وَهُوَ الصَّادِقُ الْمَصْدُوقُ: ((إِنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ أَرْبَعِينَ يَوْمًا نُطْفَةً، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يُرْسَلُ إلَيْهِ الْمَلَكُ فَيَنْفُخُ فِيهِ الرُّوحَ، وَيُؤْمَرُ بِأَرْبَعِ كَلِمَاتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ، وَأَجَلِهِ، وَعَمَلِهِ، وَشَقِيٍّ أَمْ سَعِيدٍ؛ فَوَاَللَّهِ الَّذِي لَا إلَهَ غَيْرُهُ إنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الْجَنَّةِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الْكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ فَيَدْخُلُهَا. وَإِنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الْكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الْجَنَّةِ فَيَدْخُلُهَا)) رواه البخاري ومسلم

Amesimulia Abuu 'Abdir-Rahmaan 'Abdillaah bin Mas‘uwd (رضي الله عنه): Ametusimulia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  ambaye ni mkweli mwenye kuaminiwa: “Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa mbegu (za uzazi za mama na baba), kisha arubaini zifuatazo huwa ni donge la damu, kisha arubaini zijazo huwa pande la nyama, kisha Allaah Humtuma Malaika kwake na kumpulizia roho (yake).  Na (Malaika huyo) anaamrishwa maneno manne; Kuandika rizki yake, ajali yake (umri atakaoishi duniani), amali zake, mtu muovu au mwema. Wa-Allaahi naapa kwa Yule Ambaye hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, hakika mmoja wenu huenda afanye amali za watu wa Jannah hadi ikawa baina yake na Jannah ni dhiraa na kile kilichoandikwa kikathibiti, akafanya amali ya watu wa motoni akaingia motoni. Na hakika mmoja wenu huenda afanye amali za watu wa motoni hadi ikawa baina yake na moto ni dhiraa na hapo kile kilichoandikwa kikathibiti, akafanya amali ya watu wa Jannah akaingia Jannah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

(13) Wenye kuzunguka kutafuta vikao vya Waumini wanaomdhukuru Allaah kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:

 

عن أبي هُرَيْرَة رضي اللهُ عنه، عن النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قال مَا اجتَمَعَ قَوْمٌ في بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِ اللهِ يَتْلُونَ كِتَابَ اللهِ ويَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ، إلا نَزَلَتْ عليهمُ السَّكِينَةُ، وغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمَةُ، وحَفَّتهُمُ المَلائِكَةُ، وذَكَرَهُمُ اللهُ فيمَنْ عِنْدَه))  رَوَاهُ مُسْلِمٌ 

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: Hawajumuiki watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Allaah wakisoma Kitabu cha Allaah na wakasomeshana baina yao ila watateremkiwa na utulivu na itawafunika rehma, na Malaika watawazunguka, na Allaah Atawataja kwa walio Naye.    [Muslim]  

 

Na pia:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((إِنَّ لِلَّهِ عَزَّ وَجَلَّ مَلَائِكَةً سَيَّارَةً فُضُلًا يَبْتَغُونَ مَجَالِسَ الذِّكْر، وَإِذَا وَجَدُوا مَجْلِسًا فِيهِ ذِكْرٌ قَعَدُوا مَعَهُمْ فَحَضَنَ بَعْضُهُمْ بَعْضًا بِأَجْنِحَتِهِمْ حَتَّى يَمْلَئُوا مَا بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ سَمَاءِ الدُّنْيَا، فَإِذَا تَفَرَّقُوا عَرَجُوا أَوْ صَعِدُوا إِلَى السَّمَاءِ، قَالَ : فَيَسْأَلُهُمْ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ وَهُوَ أَعْلَمُ: مِنْ أَيْنَ جِئْتُمْ؟ فَيَقُولُون:َ جِئْنَاكَ مِنْ عِنْدِ عِبَادٍ لَكَ فِي الْأَرْضِ يُسَبِّحُونَكَ وَيُكَبِّرُونَكَ وَيَحْمَدُونَكَ وَيُهَلِّلُونَكَ وَيَسْأَلُونَكَ، قَالَ: وَمَاذَا يَسْأَلُونِي؟ قَالُوا: يَسْأَلُونَكَ جَنَّتَكَ، قَالَ: وَهَلْ رَأَوْا جَنَّتِي؟ قَالُوا: لَا أَيْ رَبِّ، قَالَ: فَكَيْفَ لَوْ قَدْ رَأَوْا جَنَّتِي؟ قَالُوا: وَيَسْتَجِيرُونَكَ ، قَالَ: مِمَّ يَسْتَجِيرُونِي؟ قَالُوا: مِنْ نَارِكَ يَا رَبِّ، قَالَ: وَهَلْ رَأَوْا نَارِي؟ قَالُوا: لَا، قَالُوا: وَيَسْتَغْفِرُونَكَ، قَالَ: فَيَقُول:ُ قَدْ غَفَرْتُ لَهُمْ وَأَعْطَيْتُهُمْ مَا سَأَلُوا وَأَجَرْتُهُمْ مِمَّا اسْتَجَارُوا، قَالَ: فَيَقُولُونَ: رَبِّ فِيهِمْ فُلَانٌ عَبْدٌ خَطَّاءٌ إِنَّمَا مَرَّ فَجَلَسَ مَعَهُمْ،  قَالَ: فَيَقُولُ قَدْ غَفَرْتُ لَهُمْ هُمْ الْقَوْمُ لَا يَشْقَى بِهِمْ جَلِيسُهُمْ)) البخاري , مسلم , الترمذي والنسائي

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah (عزّ وجلّ) Anao Malaika chungu nzima ambao wanakwenda huku na kule wakitafuta vikao vya kumdhukuru Allaah, na wanapopata kikao, wanakaa na watu hao huku wakikunja mbawa zao baina yao, na kuijaza sehemu ya baina yao na uwingu wa dunia. (Watu) wanapoondoka, (Malaika) hupanda mbinguni. Akasema (Nabiy): Hapo tena Allaah (عزّ وجلّ) Huwauliza ijapokuwa Anayajua yote: “Mnatoka wapi?” Wao hujibu: “Tunatoka kwa baadhi ya waja wako duniani, walikuwa wanakusabbih na kukabbir na kuhallil na kukuhimidi na wanakuomba fadhila Zako.” (Allaah) Husema: “Wananiomba nini?” (Malaika hujibu): “Wanakuomba Jannah Yako. (Allaah) Husema: “Wameiona Jannah Yangu?”  Husema: “La, Ee Rabb”. (Allaah) Husema: “Ingekuwaje kama wangaliona Jannah Yangu!?”  (Malaika) Husema: “Wanaomba himaya Yako”. (Allaah) Husema: “Wanataka kuhamiwa kutokana na nini Kwangu?” (Malaika) Husema: “Kutokana na Moto Wako ee Rabb”. (Allaah) Husema: “Je, wameuona Moto Wangu?”  Husema: “La.” (Allaah) Husema: “Je, ingekuwaje kama wangeuona Moto Wangu!?” Husema: “Wanaomba maghfirah Yako”. (Allaah) Husema: “Nimewaghufuria na Nimewapa himaya ya yale wanayotaka wahamiwe.” (Malaika) husema: “Ee Rabb! Miongoni mwao yumo fulani, mja wako muovu ambaye alikuwa akipita tu na akakaa nao.” (Allaah) Husema: “Nimewaghufuria wote (pamoja naye), hao ni watu ambao akaaye nao hataadhibiwa.” [Al-Bukhaariy, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]

 

 

(14) Walio pamoja na Waumini waliohifadhi Qur-aan wanaojifunza Qur-aan:

 

عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((الْمَاهِرُ بِالْقُرْآنِ مَعَ السَّفَرَةِ الْكِرَامِ الْبَرَرَةِ، وَالَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَيَتَتَعْتَعُ فِيهِ، وَهُوَ عَلَيْهِ شَاقٌّ لَهُ أَجْرَانِ)) البخاري ومسلم

Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Yule aliyekuwa hodari wa kusoma Qur-aan atakuwa pamoja na Malaika Waandishi wa Allaah watukufu watiifu, na yule ambaye anaisoma Qur-aan kwa mashaka na huku anajitahidi kwa kudodosa atapata ujira mara mbili.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Tafsiyr (65) na Muslim] Rejea ‘Abasa (80:15-16).

 

 

(15) Wanaosimamia milima: 

 

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، أَخْبَرَنَا ابْنُ وَهْبٍ، قَالَ أَخْبَرَنِي يُونُسُ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، قَالَ حَدَّثَنِي عُرْوَةُ، أَنَّ عَائِشَةَ ـ رضى الله عنها ـ زَوْجَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم حَدَّثَتْهُ أَنَّهَا قَالَتْ لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم هَلْ أَتَى عَلَيْكَ يَوْمٌ كَانَ أَشَدَّ مِنْ يَوْمِ أُحُدٍ قَالَ ‏ "‏ لَقَدْ لَقِيتُ مِنْ قَوْمِكِ مَا لَقِيتُ، وَكَانَ أَشَدُّ مَا لَقِيتُ مِنْهُمْ يَوْمَ الْعَقَبَةِ، إِذْ عَرَضْتُ نَفْسِي عَلَى ابْنِ عَبْدِ يَالِيلَ بْنِ عَبْدِ كُلاَلٍ، فَلَمْ يُجِبْنِي إِلَى مَا أَرَدْتُ، فَانْطَلَقْتُ وَأَنَا مَهْمُومٌ عَلَى وَجْهِي، فَلَمْ أَسْتَفِقْ إِلاَّ وَأَنَا بِقَرْنِ الثَّعَالِبِ، فَرَفَعْتُ رَأْسِي، فَإِذَا أَنَا بِسَحَابَةٍ قَدْ أَظَلَّتْنِي، فَنَظَرْتُ فَإِذَا فِيهَا جِبْرِيلُ فَنَادَانِي فَقَالَ إِنَّ اللَّهَ قَدْ سَمِعَ قَوْلَ قَوْمِكَ لَكَ وَمَا رَدُّوا عَلَيْكَ، وَقَدْ بَعَثَ إِلَيْكَ مَلَكَ الْجِبَالِ لِتَأْمُرَهُ بِمَا شِئْتَ فِيهِمْ، فَنَادَانِي مَلَكُ الْجِبَالِ، فَسَلَّمَ عَلَىَّ ثُمَّ قَالَ يَا مُحَمَّدُ، فَقَالَ ذَلِكَ فِيمَا شِئْتَ، إِنْ شِئْتَ أَنْ أُطْبِقَ عَلَيْهِمِ الأَخْشَبَيْنِ، فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم بَلْ أَرْجُو أَنْ يُخْرِجَ اللَّهُ مِنْ أَصْلاَبِهِمْ مَنْ يَعْبُدُ اللَّهَ وَحْدَهُ لاَ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا ‏"‏‏.‏

Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها) Mke wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Nilimuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Hivi imekupitia siku iliyo ngumu zaidi ya siku ya Uhud? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Nimepata mateso niliyoyapata kutoka kwa jamaa zako, na mateso zaidi niliyoyapata kwao ni siku ya ‘Aqabah, pale nilipojipeleka mwenyewe kwa Ibn ‘Abd Yaaliyl ibn ‘Abd Kulaal. Hakunikubalia nilichokitaka. Nikaondoka sielewi niendako, sikuzinduka isipokuwa nilipokaribia Qarn Ath-Tha‘alib, nikainua kichwa changu nikaliona wingu limenifunika, nikaangalia nikamkuta humo Jibriyl, akaniita akasema: Hakika Allaah Ameisikia kauli ya watu wako kwako na jibu walilokupa, na Amekuletea Malaika wa milima ili umuamuru unachotaka katika adhabu kuwafikia jamaa zako. Akaniita Malaika wa milima, akanisalimia, kisha akasema: Ee Muhammad! Akasema: Ikiwa ni katika unachokitaka niwafunike kwa milima miwili. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: Bali nataraji Allaah atawatoa migongoni mwao watakao mwabudu Allaah Peke Yake, hawamshirikishi na chochote.” [Al-Bukhaariy]

 

 

(16) Wanaozunguka Bayt Al-Ma’muwr kama ilivyothibiti katika Hadiyth ndefu ya safari ya muujiza; Al-Israa Wal-Mi’raaj pindi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipofika mbingu ya saba ambako alimuona huko Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) akapandishwa mpaka Bayt Al-Ma’muwr Akasema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): 

 

فَرُفِعَ لِيَ الْبَيْتُ الْمَعْمُورُ، فَسَأَلْتُ جِبْرِيلَ فَقَالَ هَذَا الْبَيْتُ الْمَعْمُورُ يُصَلِّي فِيهِ كُلَّ يَوْمٍ سَبْعُونَ أَلْفَ مَلَكٍ، إِذَا خَرَجُوا لَمْ يَعُودُوا إِلَيْهِ آخِرَ مَا عَلَيْهِمْ،

 

“Nikafika kwa Ibraahiym nikamsalimia naye akasema: Unakaribishwa ee katika kizazi changu na Nabii. Nikanyanyuliwa Baytul-Ma‘muwr. Nikamuuliza Jibriyl (عليه السّلام) kuhusu hiyo. Akanijibu: Hii ni Bayt Al-Ma’muwr. Kila siku humo wanaswali Malaika sabiini elfu, wakishatoka hawarudi tena.” [Al-Bukhaariy]

 

 

(17) Wanaowaombea Waumini maghfirah. Rejea Ghaafir (40:7), Ash-Shuwraa (42:5).

 

(18) Wanaowaswalia Waumini ambao wanamswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Rejea Al-Ahzaab (33:56).

 

 

(19) Wanaowaskiliza Waumini wanaposoma Qur-aan:

 

 

عن أُسَيْدَ بْنَ حُضَيْرٍ بَيْنَمَا هُوَ لَيْلَةً يَقْرَأُ فِي مِرْبَدِه، إِذْ جَالَتْ فَرَسُهُ، فَقَرَأَ ثُمَّ جَالَتْ أُخْرَى، فَقَرَأَ ثُمَّ جَالَتْ أَيْضًا. قَالَ أُسَيْدٌ: "فَخَشِيتُ أَنْ تَطَأَ يَحْيَى فَقُمْتُ إِلَيْهَا فَإِذَا مِثْلُ الظُّلَّةِ فَوْقَ رَأْسِي فِيهَا أَمْثَالُ السُّرُجِ عَرَجَتْ فِي الْجَوِّ حَتَّى مَا أَرَاهَا". قَالَ: "فَغَدَوْتُ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ بَيْنَمَا أَنَا الْبَارِحَةَ مِنْ جَوْفِ اللَّيْلِ أَقْرَأُ فِي مِرْبَدِي إِذْ جَالَتْ فَرَسِي". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((اقْرَأْ ابْنَ حُضَيْرٍ)) قَالَ: "فَقَرَأْتُ ثُمَّ جَالَتْ أَيْضًا". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((اقْرَأْ ابْنَ حُضَيْرٍ)) قَالَ: "فَقَرَأْتُ ثُمَّ جَالَتْ أَيْضًا". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((اقْرَأْ ابْنَ حُضَيْرٍ)) قَالَ: "فَانْصَرَفْتُ وَكَانَ يَحْيَى قَرِيبًا مِنْهَا خَشِيتُ أَنْ تَطَأَهُ, فَرَأَيْتُ مِثْلَ الظُّلَّةِ فِيهَا أَمْثَالُ السُّرُجِ عَرَجَتْ فِي الْجَوِّ حَتَّى مَا أَرَاهَا". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((تِلْكَ الْمَلَائِكَةُ كَانَتْ تَسْتَمِعُ لَكَ وَلَوْ قَرَأْتَ لَأَصْبَحَتْ يَرَاهَا النَّاسُ مَا تَسْتَتِرُ مِنْهُمْ))

Amesimulia Usayd bin Khudhwayr (رضي الله عنه) kwamba alipokuwa akisoma akiwa katika mirbad yake, farasi wake alishtuka. Akasoma, akashtuka tena, akasoma akashtuka tena. Akasema Usayd: Nikaogopa asije kumkanyaga Yahyaa (mwanawe). Nikainuka kumwendea (farasi) nikaona kitu kama kivuli juu ya kichwa changu kama kina kandili kikipanda mbinguni hadi kikapotea. Nikamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) asubuhi yake nikamwambia: Ee Rasuli wa Allaah, jana usiku nilipokuwa katika mirbad yangu nikisoma Qur-aan, farasi wangu alishtuka! Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ungeliendelea kusoma Ibn Khudhwayr.” Akasema: Nilisoma lakini alishtuka tena. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ungeliendelea kusoma Ibn Khudhwayr.” Akasema: Nilisoma lakini alishtuka tena. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ungeliendelea kusoma Ibn Khudhwayr.” Akasema niliondoka kwani Yahyaa alikuwa karibu naye, nikakhofu asimkanyage. Nikaona kama kivuli kikiwa na taa kinapanda juu hadi kikapotea. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hao ni Malaika walikuwa wakikusikiliza, lau ungeliendelea kusoma hadi asubuhi, watu wangeliwaona wazi wazi bila pazia.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Mirbad ni makazi ya mifugo ya farasi au ngamia.

 

 

(20) Malaika sabiini walioteremsha Suwrah Al-An’aam (6):

 

Rejea utangulizi wa Suwrah Al-An’aam namba (6), Hadiyth iliyotajwa katika Fadhila za Suwrah hiyo tukufu.

 

 

(21) Malaika walioteremshwa kuwasaida Waumini katika vita:

 

Rejea Aal-‘Imraan (3:124-125), Al-Anfaal (8:9-12).

 

Na wengineo ila hao ndio tuliojaaliwa kuwataja.

 

 

[20] Hoja Mojawapo Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwa Hana Mwana:

 

Tafsiyr:

 

Sema ee Rasuli Mtukufu kuwaambia wale waliosema kuwa Allaah Ana mtoto ilhali Yeye ni Mmoja Pekee, Mwenye kukusudiwa kwa haja zote, Ambaye Hakujifanyia mke wala mtoto, na wala Hakuwa mwenye kufanana na chochote kile.:

 

فَأَنَا أَوَّلُ الْعَابِدِينَ﴿٨١﴾

Basi mimi ningekuwa wa mwanzo katika waja (Wake).

 

Nitakuwa mimi wa  mwanzo kumuabudia  huyo mtoto, kwa sababu atakuwa ana sehemu ya baba yake, na mimi ndio wa kwanza katika viumbe katika swala la kufuata mambo Anayoyapenda Allaah. Lakini mimi (kutokana na haya) ni wa mwanzo katika wapingaji, na mkali wao kwa kupinga. Kwa hapo sasa, ndio ikatambulika kubatilika kwake, na hii ni hoja kubwa kwa wale wanaotambua hali za Rusuli wa Allaah, na kwamba ikishatambulika kwamba wao ndio waliokamilika katika viumbe, na kwamba kila jambo la kheri basi wao watakuwa ni wa mwanzo katika kulikamilisha, na kila jambo la shari basi wao watakuwa wa mwanzo kuliacha, kulipinga, na kujitenga nalo, na lau angekuwa Allaah Ana mtoto wa kweli, basi angekuwa Muhammad Bin ‘Abdillaah ambaye ni mbora wa Rusuli kuwa wa mwanzo kumuabudia, na wala asingemtangulia yeyote yule katika washirikina.

 

Na inawezekana maana ya Aayah kuwa ni:

 

Lau Allaah Angekuwa na mtoto, basi mimi ningekuwa wa mwanzo kumuabudia Allaah, na katika ibaada yangu kwa Allaah ni kuthibitisha Alichokithibitisha, na kukanusha Alichokikanusha. Na hii ni katika ibaada ya matendo ya kiitikadi, na italazimu kutokana na maelezo haya, lau yangekuwa maneno ya kweli, basi ningekuwa mtu wa mwanzo kuthibitisha. Ikafahamika kwa maelezo haya kubatilika kwa madai ya washirikina na kuharibika kwake kiakili na kinukuzi. [Tafsiyr Al-Muyassar]

 

Ningelikuwa wa mwanzo wanaokanusha madai yenu na wa mwanzo kuamini kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Hana mwana. [Tafsiyr Atw-Twabariy]

 

Na Rejea Yuwnus (10:94) kwa faida ziyada.

 

[21] Allaah Ndiye Ilaah (Mwabudiwa Wa Haki) Mbinguni Na Ardhini.

 

Rejea Al-An’aam (6:3) kwenye maelezo bayana.

 

Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Ilaahi Mwenye kuabudiwa, na viumbe vyote vinatambua Uungu Wake, ni sawa vitake kwa khiyari, au visitake, na Uungu Wake huu pamoja na mapenzi ya viumbe Kwake, umetanda mbinguni na ardhini. Ama Mwenyewe (Allaah), Yeye Yupo juu ya ‘Arsh Yake, Yuko juu ya Viumbe Vyake, Yu Pekee kwa Utukufu Wake, na kwa Ukamilifu Wake, Ameweka madhubuti (kwa Hikma Yake) kila Alichokiumba, na kila Aliloliwekea sharia, basi sharia hiyo ni madhubuti. Hajaumba kitu isipokuwa kwa hikmah, na Haweki sharia kwa jambo lolote isipokuwa kwa Hikmah, na Hukmu Yake ya kiqadari, kisharia na kimalipo, imekusanya ndani yake hikmah. Na Allaah ni Mjuzi wa kila kitu, Anajua siri na yaliyojificha, na wala hakifichikani Kwake hata kiwe kidogo uzito wa punje ya mbegu kwenye ulimwengu wa juu au wa chini, wala ndogo yake au kubwa. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

 

[22] Waabudiwa Wa Washirikina, Hawana Uwezo Wa Kumiliki Ash-Shafaa’ah (Uombezi)

 

Yaani: Kila anaemuomba asiekuwa Allaah katika Manabii na Malaika na wasiokuwa hao, (waombwa hawa) hawamiliki ash-shafaa’ah (uombezi), na wala hawaombi isipokuwa kwa Idhini ya Allaah, na hawamwombei shafaa’ah hiyo isipokuwa yule tu aliyeridhiwa na Allaah. Na kwa sababu hii ndio Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

 

  إِلَّا مَن شَهِدَ بِالْحَقِّ  

Isipokuwa yule aliyeshuhudia.

  

Yaani: Aliyetamka kwa ulimi wake, akakiri kwa moyo wake, na akawa anatambua alichokishuhudia (huyu ndiye aliyeridhiwa na Allaah). Isitoshe, inashartiwa ushuhuda wake huu uwe kwa haqq kwamba Allaah (عزّ وجلّ) Ni Mmoja Asiye na mshirika, na Rusuli Wake Amewatuma kwa watu na Risala, na waliyokuja nayo hayana shaka yoyote ndani yake katika misingi ya Dini na matawi yake, ukweli wake na sharia zake. Hawa ndio utakaowanufaisha uombezi wa watakaopewa idhini ya kuomba shafaa’ah (uombezi), na hawa ndio watakaookoka na Adhabu ya Allaah, ndio wenye kupata thawabu zake. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

[23] Washirikina Waliamini Tawhiyd Ya Ar-Rubuwbiyyah Lakini Walikanusha Tawhiyd Ya Al-Uluwhiyyah:

 

Rejea Suwrah hii Az-Zukhruf (43:9).

 

Share