37-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْوَكِيلُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الْوَكِيلُ

 

 

الْوَكِيلُ

Al-Wakiyl

Mtegemewa Kwa Yote, Msimamizi

 

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Mwenye jukumu la kupanga mambo ya viumbe kulingana na Elimu Yake, nguvu kamili na kila Hikmah inayozunguka. Allaah (عز وجل) ni Pekee Anayewatazama marafiki Wake na kuwarahisishia mambo, kuwahifadhi dhidi ya uovu na kuwatoshelezea mambo yao yote. Hivyo, mwenye kumtegemea, Yeye humtosheleza.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 اللَّـهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۖ  

Allaah ni Mlinzi Msaidizi wa wale walioamini, Anawatoa kutoka katika viza na kuwaingiza katika nuru. [Al-Baqarah (2): 257]

 

Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ فَاعْبُدُوهُ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ ﴿١٠٢﴾

Huyo kwenu Ndiye Allaah, Rabb wenu. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye Muumbaji wa kila kitu, basi mwabuduni Yeye Pekee. Naye juu ya kila kitu ni Mdhamini Anayetegemewa kwa yote. [Al-An’aam (6): 102]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿٣﴾

Na tawakali kwa Allaah, na Anatosheleza Allaah kuwa ni Mdhamini. [Al-Ahzaab (33): 3]

 

 

 

 

Share