Vibiskuti Vya Kuyayuka Mdomoni

Vibiskuti Vya Kuyayuka Mdomoni

 

 

 

Vipimo

 

Unga wa cornstarch  - 1 Kikombe

Unga wa Ngano   - 3/4 Kikombe+1 Kijiko Cha Chakula

Chumvi   1/4 Kijiko Cha Chai

Siagi  iliolainika  -   250gm.

Sukari Ya Icing -    1/2 Kikombe

Vanilla  - 1 kijiko Cha Chai

 

Namna Ya  Kutayarisha Na Kupika

  1. Katika bakuli la kiasi,chunga cornstarch,unga na chumvi,weka kando.
  2. Koroga siagi na sukari kutumia mashine mpaka iwe laini.
  3. Weka vanilla,kisha mchanganyiko wa unga na huku unakoroga hadi uwe umeshikamana.
  4. Kanda unga kidogo kisha sukuma kama chapati,lakini sio nyembamba sana.
  5. Kisha tumia kidude cha kutolea desini unayotaka na zipange katika treya.
  6. Ziweke kwa firigi kwa muda wa nusu saa,ili zisienee wakati wa kupika.
  7. Pika (bake) kwenye oven lenye moto wa 375F kwa muda wa dakika 10-12.
  8. Toa kwenye oven na uwache bisikuti zipowe.Ukipenda chunga sukari ya icing juu kwa umaridadi.

Kidokezo:

Unaweza kusaga sukari ya kawaida kwenye blenda ikawa sukari ya icing.

 

 

 

 

 

 

 

 

Share