Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Buibui Na Njiwa Kwenye Pango La Ath-Thawr Wakati Wa Hijrah Ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)

Buibui Na Njiwa Kwenye Pango La Ath-Thawr  Wakati Wa Hijrah Ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaahu)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

Je, ni kweli katika pango la Thawr alilojificha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na Abu Bakr (Radhwiya Allaahu ‘anhu), wakati wa Hijrah kulikuwa na nyumba ya Buibui na Njiwa?

 

 

 

JIBU:

 

Huu ni uongo hakuna usahihi wowote kwenye hili!

 

 

Ni kweli kila Mwana-Aadam, akiona nyumba ya Buibui na pembeni yake akamuona Njiwa naye amekaa, akiwaona tu atasema kuwa hapana mtu hapa.

 

 

Lakini Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Alitia upofu kwenye macho ya makafiri ili wasimuone, ndio maana hata Abu Bakr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alisema: “Ee Rasuli wa Allaah, lau mmoja wao angeangalia chini ya nyayo zake angetuona!” Hivyo ni  kwa sababu hapakuwa na kizuizi chochote kile.

 

Hivyo basi hakuna usahihi kuwa Buibui na Njiwa kutajwa kwao kwenye suala la kujificha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  katika pango la Thawr.

 

 

[Fataawaa Muhammad bin Swaalih Al-‘Uthaymiyn- Liqaau Baab Al-Maftuwh 229]

 

 

Share