10-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuomba Ruhusa na Adabu Zake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب الاستئذان وآدابه

10-Mlango Wa Kuomba Ruhusa na Adabu Zake

 

Alhidaaya.com

 

 

قَالَ الله تَعَالَى:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَدْخُلُوا بُيُوتًا غَيْرَ بُيُوتِكُمْ حَتَّىٰ تَسْتَأْنِسُوا وَتُسَلِّمُوا عَلَىٰ أَهْلِهَا ۚ  ﴿٢٧﴾

Enyi walioamini! Msiingie nyumba zisizokuwa nyumba zenu mpaka muombe ruhusa na muwatolee salamu wenyewe. [An-Nuwr: 27]

 

وَإِذَا بَلَغَ الْأَطْفَالُ مِنكُمُ الْحُلُمَ فَلْيَسْتَأْذِنُوا كَمَا اسْتَأْذَنَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ  ﴿٥٩﴾

Na watoto miongoni mwenu watakapofikia baleghe, basi waombe idhini (wakati wote) kama walivyoomba idhini wale wa kabla yao. [An-Nuwr: 59]

 

 

Hadiyth – 1

عن أَبي موسى الأشعري رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( الاسْتِئْذَانُ ثَلاثٌ ، فَإنْ أُذِنَ لَكَ وَإِلاَّ فَارْجِعْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kubisha hodi ni mara tatu, ukiruhusiwa ingia na ikiwa vinginevyo basi urudi." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]

 

 

Hadiyth – 2

وعن سهلِ بنِ سعدٍ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّمَا جُعِلَ الاسْتِئذَانُ مِنْ أجْلِ البَصَرِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Sahl bin Sa'd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika kuomba ruhusa kumefanywa ili mtu asichungulie." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na An-Nasaai]

 

 

Hadiyth – 3

وعن رِبْعِيِّ بن حِرَاشٍ ، قَالَ : حَدَّثَنَا رَجُلٌ مِنْ بَنِي عَامِرٍ أنَّهُ اسْتَأذَنَ عَلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ في بيتٍ ، فَقَالَ : أألِج ؟ فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم لِخَادِمِهِ : (( أُخْرُجْ إِلَى هَذَا فَعَلِّمهُ الاسْتِئذَانَ ، فَقُلْ لَهُ : قُلِ : السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ ، أأدْخُل ؟ )) فَسَمِعَهُ الرَّجُلُ ، فَقَالَ : السَّلامُ عَلَيْكُمْ ، أَأَدْخُل ؟ فَأذِنَ لَهُ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم فدخلَ . رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .

Imepokewa kutoka kwa Rib'iyy bin Hiraash (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Alituhadithia mtu kutoka katika ukoo wa 'Aamir (Bani 'Aamir) kwamba alitaka ruhusa kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa nyumbani kwake, akasema: "Je, niingie (A-alij)?" Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia mtumishi wake: "Nenda kwa huyu mtu umuelimishe namna ya kutaka ruhusa, umwambie: "Sema: Assalaamu 'Alaykum, je niingie (A-adkhul)?" Akasikia yule mtu, naye akasema: "Assalaamu 'Alaykum, (A-adkhul) je, niingie?" Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimruhusu, naye akaingia." [Abu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 4

عن كِلْدَةَ بن الحَنْبل رضي الله عنه ، قَالَ : أتَيْتُ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، فَدَخَلْتُ عَلَيْهِ وَلَمْ أُسَلِّمْ ، فَقَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( ارْجِعْ فَقُلْ : السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ ، أَأَدْخُل ؟ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwake Kildah bin Al-Hanbal (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Nilikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na nikaingia bila kutoa salamu. Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Rudi na useme: Assalaamu 'Alaykum, (Aadkhul) je, niingie?" [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

 

Share