Skip navigation.
Home kabah

Mkate Wa Mayai

 

 

 

Vipimo

·         Mayai 4

·         Sukari ¼  Kikombe

·         Unga wa Ngano Vijiko 5 ½ vya chakula

·         Hiliki ya kusaga ½  kijiko cha chai

·         Baking powder  ½  Kijiko cha chai

·         Zabibu kavu  ¼  kikombe

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Chukua bakuli la kiasi, weka sukari, hiliki na vunja juu yake mayai  yote manne.
  2. Changanya sukari,  hiliki na mayai   kwa kutumia mashine ya kukorogea keki (cake mixer), mpaka sukari ivurugike yote na kuumuka.
  3. Washa jiko lako (oven) 350F lianze kupata moto.
  4. Weka baking powder kwenye unga na uanze kuuchanganya kidogo kidogo kwenye mchanganyiko  wa mayai na sukari. Hakikisha kila ukiweka unga kidogo unauchanganya vyema usiwe na madonge.
  5. Mimina unga  ndani ya sufuria ya kuchomea keki ya kiasi.
  6. Tupia zabibu  juu ya mchanganyiko wako.
  7. Ingiza sufuria   ndani ya jiko (oven) kwa dakika 20 kisha utoe.
  8. Uhakikishe mkate wako kama umeiva kwa kijiti cha kuchomea mshikaki au toothpick. Ingiza kijiti  katikati ya mkate kisha kitoe na ukiguse uangalie kama kikavu mkate umeiva kama bado kuna ubichi basi rudisha mkate kwa dakika 5 nyingine kisha ukague.
  9. Wacha mkate upoe kisha utoe ndani ya sufuria na uweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

Assalm akeykum

Assalm akeykum warahmatullah.
This bread is so delicous trie it plz

asalam aleykum

asalam aleykum warahmatllah...shukran kwa kutujuza ili tuweze kuhudumia ndoa zetu inshaallah jazaa yenu iko kwa allah...
ila ningependa kujua na kuuliza kwamba nimejaribu kuupika hu mkate ila haukutokea uzuri jee unauacha uumuke mara mbili?? niliacha ikaumuka sukari pamoja na mayai na hamira nilipoanza kuchanganya na unga na baking powder nilikuwa nishawasha jiko moja kwa moja nikauchoma ila kati kati ulikuwa umejirudi yaan ulikuwa haukuvimba juu kati kati uliganda sasa jee tatizo nilipi ningependa kuujua kuupika na nitajitahid naomba mnijuze...

Assalam Alykum. Asanteni

Assalam Alykum.
Asanteni sana ndugu zangu waislam kwa msaada wenu Allah atakulipeni jazaa yenu.

Naona hapo juu mumesema hamira lakini katika list ya mahitaji(utayartishaji) hamna hamira.

Naomba nifahamishwe

Shukran

asalam alaykum hamira gani

asalam alaykum

hamira gani you recommend ama ni best for mkate wa mayai na 51/2 kijiko cha chakula ni ngani?

Wa 'alaykumus-salaam wa

Wa 'alaykumus-salaam wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuh

Hamira yoyote unaweza kutumia madamu si ya zamani sana.

Kijiko cha chakula kwa maana kijiko cha supu au kinachotumiwa kulia.

Ndugu zako
AL HIDAAYA

Nurein he tamu sana

Nurein he tamu sana

Rudi Juu