Mwanamke Wa Kiislam: Hadhi Yake Katika Ummah
Shaykh 'Abdul-'Aziyz Ibn Baaz (RahimahuLlaah) [1]
Imefasiriwa na Iliyasa Hamza Maulana
"NAKALA MUHIMU"
Siri ya umuhimu wa mwanamke wa Kiislam inatanda katika mzigo mkubwa na jukumu ambao alilowekewa mbele yake, na mashaka ambayo yako katika mabega yake. Jukumu na mashaka ambayo hata mengine mwanamme anaweza kubeba.
Hadhi ya mwanamke katika Uislam ina cheo kikubwa na iliyo na taadhimu, na taathira yake ni kubwa mno katika maisha ya kila Muislamu. Kwa kweli mwanamke wa Kiislamu ni mwalimu wa kwanza katika kujenga jamii njema, ikiwa
Mtume Muhammad (Swalla Allaahu alayhi wa sallam) amesema: "Nakuachieni vitu viwili, hamtapotea kamwe
Siri ya umuhimu wake umetanda katika kazi yake nzito na mamlaka ambayo yamewekwa juu yake, na shida ambazo anabeba mabegani kwake - mamlaka na dhiki ambazo hata mwanaume hawezi kuzibeba. Ndio maana imelazimishwa kwa mtu kuonyesha hisani kwa mama yake, kuonyesha upole na uhusiano wa ukaribu ulio mzuri kwake. na katika jambo hili, apewe ubora kuliko baba mtu. Mwenyezi Mungu Mtukufu kasema:
"Na Tumemuusia mtu kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili. (Tumemuusia): Nishukuru Mimi na wazazi wako. Ni Kwangu Mimi ndiyo marudio." [Surah Luqmaan 31:14].
Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kasema,
"Na Tumemuusia mwanaadamu awatendee wema wazazi wake wawili. Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu, na akamzaa kwa taabu. Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini". [Surah Ah'qaaf 41:15].
Mtu alikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu alayhi wa salam) na akasema,
"Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nani miongoni wa watu wote anastahiki uhusiano wangu wa karibu?" Mtume akajibu. "Mama yako"
Yule mtu akauliza tena, "kisha nani?" Mtume akamjibu
"Mama yako"
Yule mtu akauliza tena, "kisha nani?" Mtume akamjibu
"Mama yako"
Yule mtu akauliza tena, "kisha nani?" Mtume akamjibu.
"Baba yako" [3]
Kwahiyo haya yanasisitiza kwamba mama mtu anapewa heshima mara tatu kuliko baba mtu.
Na kuhusu mke, hadhi yake na taathira yake katika kutuliza moyo na kuliwaza imeonyeshwa wazi wazi katika Aayah Tukufu (kauli ya Allaah), katika msemo wake Mtukufu,
"Na katika Ishara Zake ni kuwa Amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri. [Suuratur-Ruum 30:21].
Al-Haafidh Ibn Kathiyr (Aliyefariki 774H) - RahimahuLLaah - alisema katika kufafanua neno ‘Mawaddah’ na ‘Rahmah’ ambayo inapatikana katika Ayaah iliyopita, anasema:
"Al-Mawaddah inamaanisha mapenzi na mahaba na Ar-Rahmah inamaniisha rehma (upole) na huruma - kama ilivyokuwa mtu anamchukuwa mwanamke ama kwa sababu ya mapenzi kwake, au kwa sababu ya mapenzi juu yake au kwa sababu ya upole na huruma juu yake, kwa kumpa mtoto kutokana na yeye..." [4]
(Ziada: soma chini kuhusu maonyo ya kuchagua mke aliyoyatoa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam).
Na jinsi mke wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Bi Khadiyjah (Radhiya Allaahu 'anha) alivyosimama kwa namna ya pekee kusaidia
"Nifunika! Nifunike!"
Kwa hiyo, (Bi Khadijah) akamfunika mpaka hofu yake ilipotokomea, baadaye Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akamuelezea Bi Khadiyjah (Radhiya Allaahu 'anha) kila kitu kilichotokea na akasema
"Naogopa juu ya kutokewa na kitu kibaya"
(Bi Khadiyjah) akamwambia,
"
Na usisahau kuhusu mama wa waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) pamoja na taathira yake. Hata Maswahaba watukufu walikuwa wanajipatia elimu ya Hadiyth kutoka kwake., na wengi katika Maswahabiyaat (wafuasi wa kike wa Rasuulu-Allaah) walijifunza vitu mbali mbali kuhusu Sharia zilizowahusu wanawake kutoka kwake.
Sina shaka ya kwamba mama yangu- Allaah Amrehemu - alikuwa na taathira makubwa juu yangu, alikuwa ananihimiza nisome, na alikuwa ananisaidia kwa
Na pia bila shaka, nyumba ambayo ina huruma, upole, upendo na kujali, pamoja na mafundisho mema ya Kiislam itamuathiri mtu. Kwa hiyo atakuwa - ikiwa Allaah atapenda - mwenye kufanikiwa katika mambo yake na katika kitu chochote - ikiwa kutafuta ilmu, biashara, kupata maisha mazuri, au vingine baada ya hivi. Kwahiyo ni Allaah peke Yake ninayemuomba Anipe mafanikio na Atuongoze sote kwenye yale ambayo Anayapenda na Anaridhia. Na Salam na Amani za Allaah zimfikie Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na familia yake, Maswahaba zake na wafuasi wake.
Kiongezo na kizingatio kutoka kwa mfasiri
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alisema kwamba mara nyingi watu huchagua mke kwa sifa nne. Katika hayo yote manne Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) anasisitiza sababu ya mwisho ambayo ni kuoa mwanamke kwa sababu ya dini yake. Mwenye dini anaweza kukufaa katika dunia yako na bila shaka akhera yako.
[1] Ni mtu ambaye anayestahili kufuatwa: Abu ‘Abdillaah, ‘Abdul-‘Aziyz bin ‘Abdillaah bin Baaz. Alizaliwa katika mji wa Riyaadh (
Makala hii ni majibu kuhusu suala maalum ambalo lilihusu cheo na hadhi ya mwanamke wa Kiislamu na imepatikana kutoka Majmu’ul Fataawaa wa Maqaalaatil Mutanawwi`ah (3/348-350) ambayo ni ya Shaykh Abu ‘Abdillaah, ‘Abdul-‘Aziyz bin ‘Abdillaah bin Baaz.
[2] Hasan: Imesimuliwa na Maalik katika al-Muwatta (2/899) na al-Haakim (1/93), kutokwa kwa Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhu). Ilithibitishwa na Shaykh al-Albaaniy katika as-Sahiyhah (Namba 1871)
[3] Imesimuliwa na al-Bukhaariy (Namba 5971) na Muslim (7/2), kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu).
[4] Tafsri ya Quriaan Tukufu (3/439) ya al-Haafidh Ibn Kathiyr
[5] Imesimuliwa na al-Bukhaariy (1/22) na Muslim (1/139), kutoka kwa masimulizi marefu yaliyopokewa kutoka kwa mama wa waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anhu)
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


