Chapati Za Hamira Na Ufuta

Vipimo
Unga 4 Mugs
Maziwa 2 Mugs Kasorobo
Chumvi kiasi
Baking Powder 1 kijiko cha chai
Hamira 1 kijiko cha chai
Unga Kama mlaini shikia na mafuta
Yai 1
Ufuta kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Changanya pamoja unga, chumvi, hamira, baking powder na maziwa. Uchanganye unga na ukande uwe mlaini vizuri.
2. Fanya madonge
3. Sukuma kila donge na upake samli na ukunje
4. Ukisha maliza sukuma daura, isiwe kubwa
5. Iwache mpaka ikisha umuka, pakaza mayai na nyunyiza ufuta kwa juu na uchome kwenye oven kwa moto wa chini, halafu washa moto wa juu iwe brown.
6. Ukisha kuutoa pakaza mafuta kidogo kwa juu kwa kutumia brush.
7. Tayari kwa kuliwa na chai au mchuzi au kitu chochote.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


