Mahamri -Maandazi Ya Kuoka (baked)

Mahamri  -Maandazi Ya Kuoka (baked)

Vipimo

Unga - 3 Magi

Maziwa ya vuguvugu (warm) - 1 Magi

Sukari - ½ Magi

Maziwa ya unga - ½ Magi

Iliki ya unga -  ¼ Kijiko cha chai

Baking powder - 1 Kijiko cha chai

Siagi iliyoyeyushwa -  1 Kikombe cha kahawa

Mafuta - 1 Kikombe cha kahawa

Viini vya mayai (yolks) - 2

Siagi au mafuta zaidi ya kupakiza

  

Vipimo Vya Hamira 

Hamira -  2 Vijiko vya supu

Unga wa ngano -  1 Kijiko cha supu

Maji- 1 ½ Vikombe vya kahawa

Sukari - 1 Kijiko cha chai

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Katika kibakuli changanya hamira, unga, maji na sukari kwa kijiko na iache iimuke kama dakika 5 hivi.
  2. Changanya vipimo viliyobakia ( isipokuwa baking powder) Katika bakuli la mashine. Kisha tia ule mchanganyiko wa hamira na uendelee kuchanganya kwa muda wa dakika 8. Halafu tia baking powder na changanya tena dakika 3 zaidi.Funika na iaache kwa dakika 5.
  3. Chukuwa treya na uipake siagi au mafuta kisha nyunyizia unga kidogo tu.
  4. Paka mikono yako mafuta ukishika mchanganyiko wa unga kwani utakuwa unanyata  mara ya kwanza.
  5. Gawanya donge la unga mara 8 sawa sawa.
  6. Kisha funika na iiache dakika 10.
  7. Halafu Sukuma kila kidonge kwa kadri ya mviringo wa nchi 5 kwa upana kisha kata mara nne.
  8. Panga mahamri katika treya na uwache nafasi ya kiasi baina kila moja.
  9. Iache iimuke pahali penye joto kwa muda wa masaa mmoja na nusu hivi.
  10. Oka (bake) katika oveni iliyokwisha kupata moto wa 180°C kwa muda wa dakika 8 au hadi igeuke rangi ya hudhurungi isiyokolea.
Share