Skip navigation.
Home kabah

Amesikia Muadhini Wa Alfajiri Hali Akiwa Anakunywa Je, Swawm Imesihi?

SWALI:

nilikuwa nakula daku nilivo maliza kula nikawa

nakunywa maji wakati naendelea kunywa maji nikasikia wanaadhini nikaendelea kunywa maji yaliomo mdomoni, je swaumu yangu imekubalika?au inabidi nilipe?naomba nijibiwe haraka,

asanteni saana.

 



JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Swawm imesihi ikiwa hali ni kamaufuatao: ulivyotaja kuwa ulisikia muadhini na huku ulikuwa umeshaanza kunywa maji. Hii ni kutokana na dalili ya usimulizi

 

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال: كان لرسول الله صلى الله عليه وسلم مؤذنان:
بلال وابن أم مكتوم .فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم ((إن بلال يؤذن بليل
فكلوا واشربوا حتى يؤذن ابن أم مكتوم))  متق عليه

Kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhuma) ambaye amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na waadhini wawili; Bilaal na Ibn Ummi Maktuum akasema: ((Hakika Bilaal anaadhini usiku (adhana ya mwanzo), basi kuleni na mnywe hadi aadhini Ibn Ummi Maktuum)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na Allaah Anajua Zaidi