Mgonjwa Wa Pumu Anatumia Dawa Ya Kupuliza Mdomoni Je, Inabatilisha Swawm?

 

Mgonjwa Wa Pumu Anatumia Dawa Ya Kupuliza Mdomoni Je, Inabatilisha Swawm?

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Mimi ni mgonjwa wa Pumu, na kila mara au kila siku zinanijia, na

zinaponijia inanibidi nitumie dawa ili nipate nafuu, dawa ninayotumia sio ya vidonge wala sindano natumia dawa ya kupuliza mdomoni ile hewa inayotoka ndio nikimeza natapa nafuu. swali langu lipo hapa je? nikitumia dawa hiyo nitakuwa sina swaum.

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Swawm yako ni sahihi In Shaa Allaah, kwani hiyo dawa ya kupuliza inaingia katika mapafu na sio chakula kinachoingia tumboni, kwa hiyo kuitumia sio miongoni mwa vitu vinavyobatilisha Swawm.

 

Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo ya mambo yanayobatiilisha na yasiyobatilisha Swawm.

 

Mambo Muhimu Mwenye Kufunga Anapaswa Ayajue Kuhusu Swawm

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share