Surah Ngapi Zilizoteremshwa Madiynah Na Ipi Ya Kwanza

SWALI:

 

Ni surah ngapi zizotemremshwa madina, na ni ipi ya kwanza? Maasalam.


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa ndugu yetu muulizaji swali.

 

Wanachuoni wametofautiana kuhusu suala la Suwrah zilizoteremka Madiynah na zile za Makkah.

Tofauti hiyo inakuja kwa Suwrah mbili (yaani Ar-Rahmaan [Suwrah ya 55) na Al-Insaan au Ad-Dahr [Suwrah ya 76]).

 

Wengine wanasema mojawapo au zote mbili zimeteremshwa Makkah na wengine wanasema Madiynah.

 

Hivyo, kwa tofauti hiyo wengine wanasema Suwrah zilizoteremshwa Madiynah ni 28, wengine 27 na wengine tena 26. ama Suwrah ya kwanza kuteremshwa Madiynah ni Al-Baqarah, ambayo kwa mpangilio wa Qur-aan ni Surah ya pili.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share