Cheuro

Cheuro 

Vipimo

Pawa  (pepeta) - 1 Kg

Dengu za vipande za manjano - 1/2 Kg

Karanga (njugu) zilokiwisha kaangwa - ¼ Kg

Korosho - ¼ Kg

Zabibu kavu - 1 Kikombe

Chips (Crisps plain) - 2 Paketi kubwa

Bizari ya manjano - 1 kijiko cha chai

Sukari - ¼ kikombe

Chumvi - Kiasi

Ndimu ya unga - 2 vijiko vya chai

Pilipili ya unga  - 1 kijiko cha supu

Majani ya mchuzi makavu (curry leaves)(yachambue) - Misongo miwili  (bunch)

Mafuta - 2 vijiko vya supu

Mafute mengine ya kukaangia dengu na pepeta katika karai - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Roweka dengu tokea usiku.
  2. Siku ya pili weka mafuta kwenye karai na kwa moto wa kiasi kaanga dengu kisha zitoe.
  3. Kisha kaanga pepeta uzito, weka kando.
  4. Kaanga  zabibu kidogo tu zitoe.
  5. Tia mafuta vijiko 2 vya supu katika kikaango (frying pan) kaanga majani ya mchuzi pamoja na bizari ya manjano.
  6. Tia kwenye bakuli kubwa vitu vyote ulivyokaanga na uchanganye , pamoja na korosho, njugu na chipsi.
  7. Nyunyuzia  sukari, ndimu ya unga, chumvi na pili pili ya unga uchanganye vyote pamoja tayari kuliwa.

 

 

Share