Kababu Za Tuna

Kababu Za Tuna

Vipimo:

Tuna - Kopo 2 

Mkate - Slesi 5

Garam masala - Kijiko 1  cha chai

Mayai - Makubwa 2

Ndimu - Kubwa 1

Kitunguu saumu(thomu) na tangawizi - Kijiko 1

Dania / Kotmiri - Kiasi

Pilipili mbichi - I kijiko cha supu

Pilipili manga - I kijiko cha chai

Chumvi - Kiasi

Mafuta ya kukaangia

Namna Ya Kutayarish Na Kupika:

  1. Kamuwa tuna utowe maji yote.
  2. Roweka slesi za mkate katika majia kisha kamua maji ubakie mkate pekee.
  3. Changanya vipimo vyote pamoja na tuna.
  4. Tengeneza umbo la duara au umbo la yai.
  5. Kaanga kama sambusa.
  6. Kisha zipange kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

 

 

 

Share