Kusuka Nywele Na Kuchanganya Na Nyuzi Inafaa?
SWALI:
Samahani kwa kuwasumbuwa kwanza natowa shukurani kwakutuonesha mtandao huyu kwa kweli unatupa elim mimi swali langu nikusu
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako dada yetu. Hakuna samahani dada yetu kwa kuuliza swali wala hakuna makosa yoyote yaliyopatikana katika ibara hiyo.
Katika mapambo ya kike yaliyokatazwa ni kuunga nywele zake kwa nywele nyingine, zikiwa ni za kweli (zake au za mwengine) au za bandia
“Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amemlaani mwenye kuunga nywele na mwenye kuungwa” (al-Bukhaariy).
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alilitilia mkazo
Huku kuungwa kwa nywele kumeitwa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa ni udanganyifu (al-Bukhaariy).
Kwa ufupi, kuunga nywele ni haramu zikiwa za kweli au za bandia nao ni udanganyifu uliokatazwa. Ama kuunga nywele kwa vitambara au nyuzi na vitu
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


