Talaka Inayotolewa Kwa Njia Ya Simu Inapita?

 

SWALI:

Nimejiozesha na mume ambaye tulikuwa na tofauti mbali mbali na jambo kubwa zaidi ni wivu na pia kutokua na nguvu za kiume kwa ajili ya matatizo hayo nikamuomba talaka kwa hiyo akaniambia kama unataka talaka nipigie simu sasa hivi na punde nikampigia siku na kuniambia nimukutaliki nikamwambia kuwa anitumie talaka maandishi kwa njia ya email akasema unataka kumuonesha nani? nikamjibu; kaka yangu basi akafunga simu na mimi sikuwasiliana nae toka siku hiyo, na mimi nimeanza eda toka siku hio, je talaka hii imepita? na kuna umuhimu wa kuwa na talaka maandishi au vipi? shukran wa jazaakom allah kul al kheir

 


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako. Hakika ni kuwa talaka inapotolewa kwa matamshi ya ana kwa ana au kupitia kwa njia ya simu basi talaka hiyo imepita bila shaka yoyote. Talaka si lazima iandikwe mbali na kuwa katika nyakati zetu za leo huwa inahitajika katika baadhi ya wizara za serikali ikiwa ni kama uthibitisho kwa masuala mbalimbali. Au endapo akatokea mume mwengine kutaka kukuoa huenda akataka kujua kwa uthibitisho kama umeachwa kweli na ushuhuda wa kihakika ni kuwa na maandishi.

Hata hivyo tufahamu kuwa hiyo talaka imepita kisheria na uanze kuhesabu Eda yako ya talaka tokea siku hiyo.

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share