Wanawake Kufuata Jeneza Na Kumswalia Maiti
SWALI:
Je inafaa kwa mwanamke kufuatia jeneze hadi misikiti na kumswaliya maiti? Jazaakumullahu kheiran
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako. Inachukiza kwa wanawake kufuata jeneza kwa kauli ya Ummu 'Atwiyah (Radhiya Allaahu 'anha) kuwa tulikatazwa kufuata jeneza na haikufanywa ni sheria kwetu sisi (Muslim).
Ama kumswalia maiti mwanamke anaruhusiwa naye kujiunga na kuswali Swalah hiyo ya jeneza.
Ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi muhimu yanayohusu mas-ala haya:
Wanawake Wanayopasa Kufanya Wakati Wa Jeneza Linapotoka
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
