Adhkaar Za Baada Ya Swalah Tasbiyh, Tahmiyd Na Takbiyr Mara 33

 

SWALI:

Assalamu Alaikum Wa Rahmatullahi Taalah Wa Barakatuh, 
kuna  mtu ameuliza swali lifutalo nami nimeona niwatumie nyinyi mlijibu. Inajulikana kuwa baada ya salah unasema  
SUBHANNA LLAHU 33TIMES,
ALHAMDULLILLAHI 33TIMES NA
ALLAHU AKBAR 33 TIMES
so suala lake yeye,JEEE INAJUZU AKAWA ASOMA HIZO ZOTE BADALA YA 33 AKAWA ANASOMA 100 TIMES each one,yaani SUBAHHANNALLAH 100 times,ALHAMDULILLAHI 100 NA ALLAH AKBAR 100  kwa kila salah zake za fardhi na sunnah? well ktk maongezi yake nikamuuliza kwa nn anasema asome 100 times?akanambia anaona kama akisoma 100 times she loosing nothing after all anasema shughuli zote hizo kama atakuwa anasoma 100timess each itam-cost abt 20min while she can spends 5hrs-8hrs a day kuangalia tv na mambo mengine so anahizi kwa nini asipoteze 20min kwa kila salah kuongea,kumsifu,na kumpwekesha allah?

 

   


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Jibu ni kwamba, ingawa ni kitendo chema kumdhukuru Allaah kwa wingi, lakini tunapaswa kufahamu kuwa vitendo vya ibaada ni tawqifiy - kwa maana vitekelezwe kama tunavyopata mafunzo kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa alihi wa sallam). 
 

Mafunzo hayo ya kumdhukuru Allaah kwa idadi ya 33 kila baada ya Swalah yamo katika dalili ya mafunzo ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa alihi wa sallam). Haikutajwa kuwa hapo baada ya Swalah tumdhukuru zaidi ya hivyo katika kutaja hizo tasbiyh, (Subhaana Allah)  tahmiyd  (AlhamduliLlaah) na takbiyr (Allaahu Akbar). Hivyo basi kufanya kinyume na idadi hiyo itakuwa ni kuyageuza mafunzo ya tuliyoletewa na mbora wa viumbe na tukaweka ufundi wetu na mwisho kuingia katika kupingana na tuliyofunzwa, na kwa maana nyingine ni kumfanya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa alihi wa sallam) kuwa hakuwa akijua umuhimu wa kuzifanya ziwe mara mia kama ndugu yetu anavyoona. Pia bila ya shaka kuna hikma ya kuwekewa idadi kadha ya adhkaar ambayo hatuwezi kujua sisi ila Mwenyewe Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Aliyempa wahyi (ufunuo) Mjumbe Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwani yeye hasemi kwa matamanio yake:

 

((وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَى)) (( إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَى))

((Wala hatamki kwa matamanio)) ((Hayakuwa haya ila ni ufunuo uliofunuliwa)) [An-Najm: 3-4]

Mfano, tumepata mafunzo ya kujua faida ya kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa adhkaar kama hizo mara 33 kabla ya kulala katika usimulizi ufuatao:

وعن أبي هريرة رضي الله  عنه أن فاطمة رضي الله تعالى عنها أتت النبي صلى الله عليه وسلم تسأله خادماً وشكت العمل، فقال صلى الله عليه وسلم: ((ألا أدلك على ما هو خير لك من خادم، تسبحين ثلاثاً وثلاثين: وتحمدين ثلاثاً وثلاثين، وتكبرّين أربعاً وثلاثين، حين تأخذين مضجعك))   أخرجه مسلم .

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Faatwimah (Radhiya Allaahu 'anha) alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kumuomba mtumishi akilalamika kazi [za nyumba]. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  akamwambia: ((Je nikupe lililo bora kuliko mtumishi? Ufanye tasbiyh mara thelathini na tatu, tahmiyd mara thelathini na tatu, takbiyr mara thelathini na nne unapokwenda kulala)) [Muslim]

Baada ya kutekeleza hayo, 'Aliy (Radhiya Allaahu 'anhu) mume wa Faatwimah alikiri maajabu na faida kubwa walizoziona ya mabadiliko ya maisha yao hata akasema kwamba hawakuwa wakiacha abadan kuleta hizo adhkaar walipokuwa wakilala.

Kwa hiyo hatuwezi sisi kujua ya hikma au mambo ya ghayb ila ni wajib wetu kusema sami'naa wa atwaa'naa (tumesikia na kutii)

Muislamu anaweza kumdhukuru Allaah (Subhaana wa Ta'ala) wakati wote apendao masaa 24 kwa siku bila hata ya kupoteza dakika moja, kwa sababu kumdhukuru Allaah hakuna kikwazo wala hakuna mipaka, sio kama ibada nyinginezo. Ndimi zetu zinatakiwa daima zishughulishwe na adhkaar. Kwa hivyo basi afanye hivyo wakati mwengine wowote hata anapokuwa anafanya kazi zake kama za nyumba n.k.

 
Ama kwenda kinyume na yale tuliyofundishwa ni jambo lisilofaa na la hatari.  
 
Anachotakiwa baada ya Swalah azisome hizo idadi kama zilivyotajwa yaani 33 - kisha atakapomaliza anaweza kubakia hapo na kuleta Adkhaar nyinginezo ima kwa idadi kama ziko kwenye dalili au kuleta bila ya idadi maalumu.   

La muhimu pia ni kwamba idadi yoyote atakayoleta katika adhkaar, anaweza kuleta bila ya kuweka idadi maalumu ikawa ndio ada yake kila siku au kila wakati fulani. Anaweza tu kuleta idadi maalumu ikiwa ipo dalili.  Tutambue kwamba mafunzo yetu yote yanapasa yatokane na dalili.
 
Kitabu cha Hiswnul Muslim kifuatacho kina dalili za idadi ya aina za dhikri kama hizo zilizotajwa.
 
Tunatumai kwamba mafunzo haya yatatekelezwa ili kupata thawabu zake bila ya upungufu kwa kufuata mafunzo ya Sunnah.
 
Na Allaah Anajua zaidi.
 
Hiswnul Muslim
 
26 Nyiradi baada ya kutoa Salam (kumaliza Swala)
 

131 Fadhila za Tasbiyh, Tahmiyd, Tahliyl, na Takbiyr

 

Na Allah Anajua zaidi

Share