Wanawake Kuvaa Swiming Costume (Nguo Za Kuogelea) Pwani Wakiwa Na Wanaume
SW
SW
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako zuri kuhusu mas-ala ya kuoga ufukweni na mavazi ya kuogelea. Mwanzo tufahamu ya kuwa Uislamu umehimiza
Hata hivyo, tufahamu kuwa Uislamu una misingi na kanuni zake kuhusu mambo tofauti. Katika kila jambo ambalo Muislamu anafanya anafaa achunge maadili ya Kiislamu.
Uislamu katika
“Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana wasiudhiwe” (33: 59).
Hakika ni kuwa mavazi ya kuogelea huwa hayana sitara kabisa. Pia tufahamu kuwa Allaah Aliyetukuka hataki wanawake wawe ni wenye kutoka ovyo ovyo
“Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani” (33: 33).
Jamaa za mume, hasa wa kiume ni watu ambao kisheria hawafai kuona uchi wako (mwanamke) na uchi mwanamke ni mwili mzima isipokuwa uso na viganja vya mkono. Ni vyema ikiwa mke hana budi kwenda beach basi asiogelee kabisa kwani atakuwa ameruka mipaka iliyowekwa na Allaah Aliyetukuka na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wala isiwe beach ya mchanganyiko wa wanawake kwa wanaume ambapo ataona wanaume waliovaa nguo za kuogelea na hivyo kuona maeneo ya uchi yao.
Tusome makala ifuatayo tuone madhara na ubaya wa kuchanginyikana wanawake na wanaume wasio Maharimu.
Ikhtilaatw (Kuchanganyika Wanaume Na Wanawake)
Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Amsaidie huyo dada yako na sisi sote katika kufuata maagizo ya sheria ya Kiislamu.
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


