Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislam - 06

 

Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislaam – 06

 

Imefasiriwa na: Naaswir Haamid

 

Alhidaaya.com

 

 

Suala Nambari 6 Linaloeleweka Vibaya

 

Uislaam unaamrisha kumuabudia mwanaadamu kwa sababu:

 

  • Waislamu ni ‘Wafuasi wa Muhammad’

 

Jibu

 

Wasio kuwa Waislamu wa kale ambao walionekana kama kwamba ni watafiti wa Uislaam waliita ‘Dini ya Muhamaadi’, wakimaanisha kwa maana nyengine kwamba Waislaam walimuabudia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hivyo, msingi wa suala hili (la uongo) ni kwamba hakika linatokana na wasiokuwa Waislaam. Hata hivyo, kama ilivyoelezwa hapo juu, ‘Muislaam’ ni “yule anayemnyenyekea Allaah”. Asili ya Uislaam ni kwenye hali ya umoja ulio safi, tena safi, safi kabisa. Allaah Anasema ndani ya Qur-aan:

 

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ﴿١﴾اللَّـهُ الصَّمَدُ﴿٢﴾لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ﴿٣﴾وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ﴿٤﴾    

 

Sema: Yeye ni Allaah Mmoja Pekee.  Allaah ni Aliyekamilika sifa za utukufu Wake, Mkusudiwa haja zote. Hakuzaa na wala Hakuzaliwa. Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye. [Al-Ikhlaasw: 1- 4]

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ ۚ أَفَإِن مَّاتَ أَوْ قُتِلَ انقَلَبْتُمْ عَلَىٰ أَعْقَابِكُمْ ۚ وَمَن يَنقَلِبْ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ فَلَن يَضُرَّ اللَّـهَ شَيْئًا ۗ وَسَيَجْزِي اللَّـهُ الشَّاكِرِينَ ﴿١٤٤﴾

 

Na Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) si yeyote isipokuwa ni Rasuli tu. Wamekwishapita kabla yake Rusuli. Je, akifa au akiuawa mtageuka nyuma ya visigino vyenu (mrudi ukafirini)? Na atakayegeuka nyuma ya visigino vyake, basi hatomdhuru Allaah kitu chochote. Na Allaah Atawalipa wenye kushukuru. [Al-‘Imraan: 144]

 

Imesimuliwa katika [Swahiyh Al-Bukhaariy] kwamba:

 

Amesimulia Mu’aadh bin Jabal: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Ee Mu’aadh! Je unatambua haki ya Allaah juu ya waja Wake?” Nikasema: “Allaah na Nabiy Wake wanajua lililo bora” Nabiy akasema: “Kumuabudia Yeye (Allaah) Pekee na bila ya kumshirikisha na chochote pamoja Naye (Allaah) kwenye ibada. Je unatambuwa haki yao juu Yake?” Nikajibu: “Allaah na Nabiy Wake wanajua lililo bora” Nabiy akasema: “Kutowaadhibu (kama wakimuabudu).” [9:93:470]

 

Amesimulia ‘Umar: Nimemsikia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Musivuke mpaka katika kunisifu kama Wakristo walivyomsifu mtoto wa Maryam, kwani mimi ni mja. Hivyo, niiteni Mja wa Allaah na Mjumbe Wake.” [4:55:654]

 

 

.../7

 

 

 

 

 

Share