Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislam - 07

 

Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislaam - 07

 

Imefasiriwa na: Naaswir Haamid

 

Alhidaaya.com

 

 

Suala Nambari 7 Linaloeleweka Vibaya

 

Uislaam unakubali kuwaua watu wasio na hatia kwa sababu:

 

  • Waislamu wanaweza kuwa ni magaidi

 

  • Waislamu wanashiriki kwenye ‘vita tukufu’ (jihaad)

 

  • Uislaam umeenea kwa panga

 

  • Ni mfumo wa kisheria ulio katili na dhalimu

 

Siku hizi, suala hili linaloeleweka vibaya ni miongoni mwa lililoenezwa mno kabisa kuhusu Uislaam. Lakini bado ndani ya Qur-aan, Allaah Anaeleza bila ya utata (tafsiri):

 

وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۗ وَمَن قُتِلَ مَظْلُومًا فَقَدْ جَعَلْنَا لِوَلِيِّهِ سُلْطَانًا فَلَا يُسْرِف فِّي الْقَتْلِ ۖ إِنَّهُ كَانَ مَنصُورًا ﴿٣٣﴾

 

Na wala msiue nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha (kuiua) isipokuwa kwa haki. Na atakayeuliwa kwa kudhulumiwa, basi Tumemfanya mrithi wake awe na mamlaka.  Lakini asipindukie mipaka katika kuua. Hakika yeye atasaidiwa (kwa shariy’ah). [Aal-‘Imraan:33]

 

Tukiegemea kwenye Aayah hii, hairuhusiki kwa Uislaam kuua mtu yeyote asiye na kosa kwa baadhi ya makosa ya jinai. Ni vyema tukakumbuka katika nukta hii, tofauti iliyofanywa hapo juu baina ya Qur-aan na Sunnah, na Waislamu; ni Qur-aan na Sunnah pekee ndizo zilizoafikiwa kuwa zinaendana pamoja na matakwa ya Allaah, wakati Waislamu wanaweza sana kutetereka. Hivyo, kama Muislamu yeyote ataua mtu asiye na hatia, Muislamu huyo ametenda dhambi mbaya kabisa, na hakika tendo hilo haliwezi kudaiwa kuwa limefanywa “kwa jina la Uislaam”.

 

Na itambulike wazi basi, kwamba “Gaidi Muislamu” inafanana na maneno mawili yenye kupewa maana tofauti ili kutoa msemo mmoja oxymoron: kwa kuua watu wasio na hatia, Muislamu anatenda dhambi kubwa, na Allaah ni anayefanywa kuwa Muadilifu personified. Msemo huu ni wa kukosa nidhamu na kuushushia hadhi Uislaam, na ni lazima uepukwe. Inategemewa kwamba; kwa vile uelewa na hamasa ya Uislaam inapanda juu kwa jamii iliyo ya kawaida ya watu, basi watu watayatenganisha mbali mbali maneno ya “ugaidi” na “Uislaam”, yasitumike ndani ya msemo mmoja.

 

Sababu nyingine inayokuzwa ili kukubaliana na suala hilo linaloeleweka vibaya ni kwamba Allaah Ameweka “jihaad” juu yetu. Tamko la “vita tukufu” linatokana na enzi za Vita vya Msalaba Crusades na limechimbuka ndani ya Uingereza kama ni kilio cha kasi dhidi ya Waislamu huko Jerusalem. Jihaad ni neno la Kiarabu lenye maana ya kupambana, lakini kwa mujibu wa maelezo ya aya nyingi ndani ya Qur-aan, linabeba maana ya mpambano wa kijeshi, au vita. Allaah Amewasilisha hatua kwa hatua wajibu wa mpambano wa kijeshi kwa jamii ya Waislamu wakati wa kipindi cha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Aayah ya mwanzo iliyoshushwa kwa mnasaba huo ni kama ifuatayo:

 

أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَاتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ ﴿٣٩﴾

 

Wameruhusiwa (kupigana) kwa wale wanaopigwa kwa kuwa wamedhulumiwa. Na kwamba Allaah bila shaka ni Muweza wa kuwanusuru. [Al-Israa: 39]

 

Aayah hii inaweka bayana masharti kabla ya kupigana vita vyovyote ndani ya Uislaam; ni lazima kuwepo masharti ya kuwepo unyanyasaji kwa watu. Allaah Ameweka wazi amri juu yetu ya kupigana dhidi ya unyanyasaji na udhalimu, hata kama ikiwa kwa gharama ya kumwaga damu kama aya ifuatayo inavyoonesha:

 

وَقَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿١٩٠﴾ وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ ۚ وَالْفِتْنَةُ أَشَدُّ مِنَ الْقَتْلِ ۚ وَلَا تُقَاتِلُوهُمْ عِندَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ حَتَّىٰ يُقَاتِلُوكُمْ فِيهِ ۖ فَإِن قَاتَلُوكُمْ فَاقْتُلُوهُمْ ۗ كَذَٰلِكَ جَزَاءُ الْكَافِرِينَ ﴿١٩١﴾

 

Na piganeni katika njia ya Allaah na wale wanaokupigeni, wala msitaadi. Hakika Allaah Hapendi wenye kutaadi. Na wauweni popote muwakutapo, na watoeni popote walipokutoeni. Na fitnah ni mbaya zaidi kuliko kuua. Na wala msipigane nao kwenye Al-Masjidil-Haraam mpaka wakupigeni humo, watakapokupigeni basi wauweni. Namna hivi ndivyo jazaa ya makafiri. Wakikoma, basi Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-Baqarah: 190-192]

 

Kama ambavyo mtu anaweza kufikiria, taratibu za mpambano wa vita umetafsiriwa wazi na kwa upana ndani ya Qur-aan na Sunnah. Kwa vile hili ni somo moja lililo kubwa mno, tunafupisha kwa urahisi sehemu moja wapo kwa kutanabahisa kwamba haifai kuua wanawake, watoto, walemavu, wazee, na walio waadilifu. Kutokana na Sunnah, hususan ndani ya somo la Sunnah linaloitwa [Swahiyh Al-Bukhaariy], tunaona:

 

Imesimuliwa na ‘AbduLlaah: Wakati wa kipindi fulani cha vita Ghazawat enzi za Nabiy, mwanamke alikutikana ameuawa. Rasuli wa Allaah hakukubaliana na kuuawa kwa wanawake na watoto.

 

Suala (jengine) linaloeleweka vibaya ambalo linahusiana na Jihaad, kawaida linatangazwa na Waislamu wanaosema kwamba “Jihaad ni kwa kuhami mipaka.” Qur-aan na Sunnah inakataa kabisa dhana hii. Kama aayah iliyonukuliwa hapo juu inavyoonesha, jihaad ni wajibu wakati wote panapotokezea dhulma (na sio tu wakati wa kuhami mipaka), na Waislamu hawahitajii matamshi ya uongo yanayotolewa duniani pale inapokuja kusimamisha wajibu huu. Kutokana na Sunnah, hususan ndani ya [Swahiyh Al-Bukhaariy]:

 

Imesimuliwa na Abuu Mussa: Mtu mmoja alikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kuuliza, “Mtu anapigana vita kwa ngawira; mwengine anapigana kwa umaarufu na wa tatu anapigana kwa kujionesha, ni yupi miongoni mwao anayepigana kwa ajili ya Allaah?” Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema, “Yule anayepigana kwa Neno la Allaah (yaani Uislaam) atakuwa bora, anayepigana kwa ajili ya Allaah.” [4:52:65]

 

Hivyo, Allaah Anatuwajibisha kupigana vita wakati wowote pale watu wanapokandamizwa vibaya hata kukosa uhuru wa kumsikiliza au kumfanyia kazi Rasuli wa Allaah kama ilivyo ndani ya Qur-aan na Sunnah.

 

Sababu ya tatu ambayo kawaida huwa inanukuliwa kuhusu suala hili linaloeleweka vibaya katika Uislaam inasema kwamba njia hii ya maisha inakubaliana na kuuwa watu wasio na hatia kwa sababu mfumo wake wa sheria ya Uislaam ni wenye ukatili usio na maana. Hoja hii ni nyepesi kwa namna mbili. Kwanza, inawafanya wanaadamu kuwa ni waadilifu na waliotakasika kuliko Allaah, na hivyo tunaweza kubadili Shariah. Pili, mara nyingi imeegemezwa kuidhania Shariah za Kiislamu ni zenye kutekelezeka kiulaini, kama vile kusema “wizi wote wanapata kukatwa mikono yao.”

 

Qur-aan na Sunnah imeweka wazi kwamba sheria ya kisasi, ni juu yetu kwa mauaji na jeraha la mwili, lakini msamaha ni bora kama aya zifuatazo kutoka Qur-aan zinavyoonesha (tafsiri):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِصَاصُ فِي الْقَتْلَى ۖ الْحُرُّ بِالْحُرِّ وَالْعَبْدُ بِالْعَبْدِ وَالْأُنثَىٰ بِالْأُنثَىٰ ۚ فَمَنْ عُفِيَ لَهُ مِنْ أَخِيهِ شَيْءٌ فَاتِّبَاعٌ بِالْمَعْرُوفِ وَأَدَاءٌ إِلَيْهِ بِإِحْسَانٍ ۗ ذَٰلِكَ تَخْفِيفٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَرَحْمَةٌ ۗ فَمَنِ اعْتَدَىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَلَهُ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٧٨﴾

 

Enyi walioamini! Mmeandikiwa shariy’ah ya kisasi kwa waliouawa; Muungwana kwa muungwana, na mtumwa kwa mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke, na anayesamehewa na nduguye kwa lolote basi kufuatilizwa kwake kuwe kwa wema na kumlipa kwake iwe kwa ihsaan. Hiyo ni takhafifu kutoka kwa Rabb wenu na rahmah. Na atakayevuka mipaka baada ya hapo basi atapata adhabu iumizayo. [Al-Baqarah: 178]

 

Pia, Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَجَزَاءُ سَيِّئَةٍ سَيِّئَةٌ مِّثْلُهَا ۖ فَمَنْ عَفَا وَأَصْلَحَ فَأَجْرُهُ عَلَى اللَّـهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ﴿٤٠﴾ وَلَمَنِ انتَصَرَ بَعْدَ ظُلْمِهِ فَأُولَـٰئِكَ مَا عَلَيْهِم مِّن سَبِيلٍ﴿٤١﴾ إِنَّمَا السَّبِيلُ عَلَى الَّذِينَ يَظْلِمُونَ النَّاسَ وَيَبْغُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ ۚ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٤٢﴾ وَلَمَن صَبَرَ وَغَفَرَ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ﴿٤٣﴾

 

Na jazaa ya uovu ni uovu mfano wake. Lakini atakayesamehe na akasuluhisha, basi ujira wake uko kwa Allaah, hakika Yeye Hapendi madhalimu. Na bila shaka anayelipiza kisasi baada ya kudhulumiwa, basi hao hawana sababu ya kulaumiwa. Hakika sababu (ya kulaumiwa) ni juu ya wale wanaodhulumu watu na wanakandamiza katika ardhi bila ya haki. Hao watapata adhabu iumizayo. Na atakayevuta subira na akasamehe, hakika hilo bila shaka ni katika mambo ya kuazimiwa.[Ash-Shuwraa: 40-43]

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ameamrisha sheria ya kisasi juu yetu Akitambuwa vilivyo kwamba tunaweza kuijadili. Ndani ya jamii nyingi za leo zisizokuwa za Waislamu, kuna majadiliano yanayoendelea kuhusu adhabu ya kifo. Kwa Uislaam, mjadala huu ni butu, Allaah Amekwishalitolea maamuzi suala hilo kwa ajili yetu. Hata hivyo, Ametupatia aayah ya ajabu ndani ya Qur-aan ambayo inatushauri kufikiria vyema suala hilo vizuri kama tunahitaji kuielewa (tafsiri inafuata):

وَلَكُمْ فِي الْقِصَاصِ حَيَاةٌ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٧٩﴾

 

Na mtapata katika kisasi (kuokoa) uhai enyi wenye akili ili mpate kuwa na taqwa. [Al-Baqarah: 179]

 

Watu wengi pia hawapo na uelewa wa sharti zilizo kali ambazo ni lazima zitimizwe kwa sheria ya kisasi kufanyiwa kazi. Sunnah imejaa mifano ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ikituonesha pale sharti za sheria ya kisasi zinapotimizwa kabla ya kufanyiwa kazi. Kwa mfano, mwizi atawajibika tu kukosa mkono wake kama bidhaa aliyoiba imevuka kiwango fulani, na kama ikithibitishwa kwamba bidhaa hiyo imehamishwa kutoka sehemu yake ya awali. Wizi wa chakula hauna adhabu ya mtu kukosa mkono wake, na bidhaa nyengine pia zimesameheka. Huu ni mfano tu wa namna sheria zinavyofanyiwa kazi kwa hadhari sana ndani ya Uislaam.

 

Mwisho, hoja nyengine inayokuzwa kwa suala hili linaloeleweka vibaya mno ni kwamba Uislaam ‘umeenea kwa panga’. Ni lazima ieleweke kwa sasa kwamba ni lazima daima tutofautishe baina ya Qur-aan na Sunnah na Waislamu pale inapofika hatua ya kutambua nini Allaah Ametuhitajia (sisi kufanya). Allaah Ameeleza wazi ndani ya Qur-aan:

 

لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ ۖ قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ ۚ فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ لَا انفِصَامَ لَهَا ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٥٦﴾

 

Hapana kulazimisha katika Dini, kwani imekwishabainika kati ya uongofu na upotofu. Basi atakayemkanusha twaghuti na akamwamini Allaah kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika, na Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote. [Al-Baqarah: 256]

 

Hivyo, Haiwezekani kukubali Uislaam kwa nguvu. Hata kama Waislamu wasio na uongofu watajaribu ‘kulazimisha’ Uislaam namna fulani kwa wengine, haitokubaliwa na Allaah kwa mujibu wa aya hii.

 

Mijadala ya taariykh ambayo inajaribu kufafanua kwamba Waislamu ‘hawajawabadili wengine kwa nguvu’ hakika ni hoja ndogo kwa mjadala uliopo hapo juu. Hata hivyo, ni vyema kubainisha kwamba (kwa mujibu wa) taariykh, Uislaam umeenea kwa njia za amani. Ujumbe wa Allaah ulifikishwa Afrika na kusini mwa mashariki ya Asia kwa wafanyabiashara walio Waislamu, na leo nchi kubwa kabisa yenye Waislamu duniani ni Indonesia. Safari za kijeshi zilizopelekea kuteka nyara kwa kuzungushia mipaka ya Ulaya na Asia ya kati, zote zilifanikiwa kwa (Uislaam) kustahamilia imani na kanuni (za dini) nyengine.

 

Kwa mara nyengine, ni muhimu kukumbuka kwamba Allaah Anatamka kwamba Haiwezekani Uislaam kulazimishwa kwa mtu, hivyo Waislamu hawaoni haja ya kujaribu!

 

 

 

.../8

 

 

 

Share