Kula Samaki Ijumaa Na Kukaribia Zinaa

SWALI:

assalam alyekum viongozi wa dini yenye haki ya Allah s.a, swali langu ni kwamba kuna aya /hadithi ya mashia nimeisikia kwamba '" mtu anayekula samaki siku ya ijumaa nanaingia peponi na nyingine usiikaribie zinaa ila kwa dharura.

 

 JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allah Mtukufu, Swalah na salamu zimfikie kipenzi chetu, Mtume Muhammad (s.a.w.w.), Ahli zake na Maswahaba wake (r.a.) na Watangu Wema na waliowafuata kwa kheri mpaka Siku ya Kiyama.

Hadiyth za Mashia ni za kwao lakini cha kufahamika ni kuwa sisi na wao tunatafautiana kabisa katika Itikadi, na vitabu wanavyotumia wao vya Hadiyth sisi hatuvitambui na wao hawawatambui kabisa Maimamu kama Al-Bukhariy, Muslim na wengineo.

Hivyo, wao wanaweza kusema chochote wanachotaka, kwao hata huyo samaki ni lazima achinjwe kabla ya kuliwa (kama wanavyosema Ma-Bohora, ambao ni tawi la kishia).

Kwa hakika katika Uislamu wa sawa hata ukiwa katika Ihramu ambapo hufai kuwinda mnyama lakini inaruhusiwa kuvua samaki. Na katika Hadiyth Sahihi hakuna kuwa ukila kitu fulani siku fulani basi wewe umepata cheti cha kuingia Peponi au ndio utaingizwa motoni.  Isipokuwa tu kwa  kula vitu ambavyo ni haramu ndio utapata dhambi.

Na kuhusu zinaa, zinaa ni zinaa wala hakuna zinaa ya dharura. Allah Ametueleza kuhusu jambo hili kiujumla pale Aliposema:

 “Wala usikaribie zinaa. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya (17: 32).

Hapa Allah Ametukataza hata kuikaribia. Hawa Mashia huwa wanajuzisha zinaa kwa jina ndoa ya muda (Mut'ah) ambayo imeharamishwa.  Na ukiangalia katika tovuti yetu hii kwenye kiungo kiufatacho, ingia utapata maelezo marefu kuhusu aina hiyo ya zinaa ambayo imepigwa marufuku na Uislamu.

Ndoa Ya Mut‘ah

Na Allah Anajua zaidi.

 

Share