Nani Mwenye Jukumu la Aqiyqah?

 

SWALI:

 

Naomba ufafanuzi juu ya nani anapaswa kumfanyia aqiyqah mtoto, kwani kuna wanaosema ni jukumu la baba (kuumeni kwa mtoto). Mama haifai kumfanyia mtoto hata kama anauwezo. Nimeuliza wiki iliyopita jawabu sijapata, nimejaribu kulisarch pia sijaliona. Naomba sana kupata uhakika wa hili.

Wabbillahi Tawfyq.

 

 


JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu 'Aqiyqah. Hakika ni kuwa jukumu la 'Aqiyqah limepatiwa baba mzazi wa mtoto. Jukumu hilo amepatiwa yeye kwa kuwa yeye ndiye mwenye kuangalia nyumba kwa chakula, mavazi, matibabu, na mengineyo.

 

 

Ikiwa baba amekufa au kwa sababu moja au nyengine hana uwezo basi, mkewe anaweza kusaidia na ujira atapata mbele ya Allaah Aliyetukuka. Kwa hivyo katika suala hili kuna wasaa na kutegemea na maelewano yenu na kusaidiana kwenu. Kusaidiana ni njia njema kwani hata Maswahabiyah waliokuwa matajiri wakiwasaidia waume zao katika mambo kadhaa.

 

 

Kwa faida zaidi katika mas-ala ya ‘Aqiyqah ingia katika viungo vifuatavyo:

 

Kufanya Aqiyqa Ni Lazima Au Sunnah?

 

‘Aqiyqah –Inafaa Kuwafanyia Watoto Wanapokuwa Wakubwa – Tofauti ‘Aqiyqah Ya Mtoto Wa Kiume Na Wa Kike

 

'Aqiyqah

 

 

Umri Anaotakiwa Mtoto Mchanga Kunyolewa Nywele

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share