Mwenye Ugonjwa Wa Ukimwi Anaweza Kufunga Ramadhwaan?

 

SWALI:

 

Assalaam aleykum wa rahmatullahi wabaraakat.Nduzanguni waislamu,shukrani sana kwenu kwa kuweza kuwasiliana nanyi na imetupa wingi wa elimu ambazo hatukuwa nazo.

swali langu ni.

-Kuna ndungu wetu ambaye anaugua na huu ugonjwa wa ukimwi,alhamdulillah ameweza kupata dawa.je, anaweza kufunga Ramadhani ama yumo katika wangonjwa wasie funga kwa ajili ya afya zao?Ramadhaan Karim

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Swawm katika hali ya ugonjwa inategemea  uwezo wa mtu. Ikiwa ataweza kufunga bila ya taklifu yoyote ya siha yake basi imewajibika kwake kufunga. Na ikiwa hawezi kufunga kwa vile italeta madhara katika siha yake basi atakuwa miongoni mwa waliopewa udhuru wa kutokufunga kutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa):

 

 

(Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine)) [Al-Baqarah:185]

 

Ni Rahma ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) kwamba Hamkalifishi mtu na jambo asiloliweza:

 

 

 

((Allaah haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo. Faida ya iliyoyachuma ni yake, na hasara ya iliyoyachuma ni juu yake pia)) [2: 286].

 

 

Atakalopasa kufanya ni  ima alipe siku za mbele ikiwa pia atakuwa na uwezo wa kufunga bila ya kuathiri siha yake au kumfanyia taklifu, ikishindikana itabidi alipe kafara kwa kulisha masikini mmoja kwa kila siku moja ya Swawm. Na Anaweza kulipa ima kulisha maskini 30 siku mbali mbali au kulisha wote kwa pamoja kwa maana wote 30 kwa siku moja. Vyovyote atakavyofanya inajuzu kwani Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ‘anhu) alifanya hivyo alipokuwa na umri mkubwa na aliposhindwa kufunga alilisha masikini siku ya mwisho ya Ramadhaan.

 

 

Tunamuombea Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) Ampe shifaa.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share