Niyyah: Hajatia Niyyah Ya Kusoma (Kutamka), Je, Swawm Yake Itakuwa Sahihi?

SWALI:

 

Swali langu nihili je nimeandaa daku yangu nikaona nijipumzishe nikalala nilipoamka alfajiri imeisha ingia na mimi sijatia ilenia yakusoma lakini moyoni mwangu nina nia yakufunga je swaumu yangu itaswihi?

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kwanza inatosheleza kabisa kuwa niyah yako ilikuwa ni kufunga kwa vile ulikuwa ushatayarisha daku, na hiyo ni dalili ya kuwa tayari ushadhamiria kufunga siku inayofuata. Kwa hiyo ungeliweza kufunga na Swawm yako ingelikuwa sahihi.

 

Ama kutia niyah kwa kutamka, hakuna mafunzo hayo katika Sunnah, bali kufanya hivyo ni bid'ah. Niyah ya ibada yoyote haitamkwi bali huwekwa moyoni. Mfano inapoadhiniwa Swalaah ya Alfajiri, ukaamka na kwenda kufanya wudhuu na kusimama kuswali au kwenda Msikitini inakuwa tayari umeshaweka niyah yako moyoni kuiswali Swalaah hiyo.

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi kuhusu nia katika ibada.

 

Vipi Kutia Niyah Ya Ibaada?

Niyah Ya Swawm Ni Kwa Kila Siku Au Mara Moja Inatosha

Vipi Kutia Niyah Ya Ibaada Kama Swawm?

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share