Jimai: Ameota Kuingiliwa Katika Kitendo Cha Ndoa, Je, Swawm Yake Ni Sahihi?

SWALI:

 

ikiwa niko katika swaumu kisha nikapitiwa na usingizi katika njozi nikaota naingiliwa nilipo amka nikajikuta nimechafuka je nisahihi kuendelea na swaumu? yanipasa nioge kama mtu aliyeingiliwa kwa kujitoharisha?

 


JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Swawm itakuwa sahihi In shaa Allaah, kwani si khiari yako hilo kukutokea. Linalokupasa ni kuoga (ghuslu) na kuendelea na Swawm yako

 

 

Na Allaah Anajua zaidi  

 

Share