Daku: Inafaa Kula Daku Siku Ya Mwanzo Kuamkia Ramadhwaan?

 

 

Inafaa Kula Daku Siku Ya Mwanzo Kuamkia Ramadhaan?

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Asalaam alaikumu waRahamatulahi wabarakatuh kwanza kabisa nipende kutoa shukran zangu kwa Allahkwa kuniwezesha kukutana tena na mwezi mtukufu wa Ramadhana hali ya kuwa ni mzima wa afya  hivyo sina budi kusema alhamdul lahi rabila alamina.Pia ngugu zangu wa watukufu waislamu wa alhidaaya nina maswali mengi ya kuwauliza ila kwa leo ninaomba mnisaidieswali lifuatalo;

siku ya kwanza ya mwezi wa Ramadhani kabla ya kuanza kufunga ninaruhusiwa kula daku?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salaau zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Inafaa kula daku siku ya mwanzo kuamkia Ramadhwaan kwani inahesabika tayari Ramadhwaan ishaingia na mapendekezo ya kula daku mtu anapotaka kufunga yapo kutokana na Hadiyth ifuatayo:

 

 (( تسحروا فإن في السحور بركة ))   رواه البخاري ومسلم  

((Kuleni daku kwani katika huko kula daku, kuna baraka)) [Al-Bukhaariy na Muslim]    

 

Kwa hiyo ni vizuri kuamka kula daku usiku wa kumakia siku ya kwanza ya Ramadhwaan.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share