Niyyah: Kuna Tofauti Baina Ya Niyyah Ya Swawm Ya Ramadhaan Na Swawm Ya Sunnah?

Kuna Tofauti Baina Ya Niyyah Ya Swawm Ya Ramadhaan Na Swawm Ya Sunnah?

 

 www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Asalam alaykum warahmatu llahi wabarakatuh

 

Shukrani zote njema zinamstahiki mola mlezi wa ulimwengu wote na sala na salamu zimshukie Mtume wetu Muhammad Swala llahu alayhi wasaalam, inshallah Mwenyezi Mungu atuzidishie baraka sote waandaaji na wapenzi wa tovuti hii.

 

Napenda kuuliza suala langu kama ifuatavyo, hivi ni kweli swaumu ya sunnah nia yake haina muda maalum, nina maana kwamba funga ya Ramadhani tunatia nia kufunga wakati wa usiku na kabla ya alfajiri, lakini hizi swala za sunna mtu anaweza kuamua tu kuwa sasa hivi nafunga hata kama ni asubuhi. Nategema kupata majibu, inshalla Mwenyezi Mungu atawafikisha kunijibu suala langu hili mapema.

wabillahi taufiki

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Swawm ya faradhi haisihi kabisa kishariy'ah kama hutotiia niyyah ya kufunga kabla ya alfajiri. Na nia mahali pake ni moyoni hakuna haja kabisa ya kuitamka.

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Vipi Kutia Niyyah Ya Ibada Kama Swawm?

 

Nia Ya Swawm Ni Kwa Kila Siku Au Mara Moja Inatosha

 

Swalah Ya Witr Inaswaliwa Vipi Na Vipi Kutia Niyyah?

 

Vipi Kutia Niyyah Swalah Za Qiyaamul-Layl?

 

Ama Swawm ya Sunnah haina haja kutia niyyah kwani hata asubuhi unaweza kutia niyyah ya kufunga ikiwa hujala kitu.

 

Ni maarufu kuwa Nabiy  Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa asubuhi wakati mwengine akipita kwenye nyumba zake akiuliza kama chakula. Akijibiwa kuwa hakuna basi alikuwa anasema kuwa mimi nimefunga. Hivyo ikiwa asubuhi bado ipo unaweza kutia nia ya kufunga Swawm ya Sunnah.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share