Bajia Za Dengu Na Viazi

Vipimo
Unga wa dengu 3 vikombe vikubwa
Chumvi 1 kijiko cha chai
Mbatata (kiazi) 1
Maji baridi 1 glass
Baking powder 1 cha chai
Kotmiri iliyokatwakatwa 4 -5 Miche
Kitunguu maji kilosagwa 2 kijiko cha supu
Thomu ilosagwa au ya unga 1 kijiko cha chai
Mafuta 500 ml
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Tumia bakuli lenye nafasi mimina unga na viungo vyote.
- Tia maji ukitumia uma au mchapo wa mkono (usotumia umeme) kuvuruga mchanganyo.
- Ukisha kuwa laini bila mavimbo, hakikisha si mzito na si uji sana (mwembamba).
- Menya kiazi na kwaruza kiwe mithili ya tambi kisha tia ndani ya unga vuruga uchanganyike.
- Uwache kwa muda wa robo saa (dakika 15) paka 20.
- Weka karai jikoni au sufuria nzito ndogo, tia mafuta na acha yapate moto sawasawa.
- Tumia kijiko cha supu kuteka unga kutia kwenye mafuta , unapotia hakikisha kipimo chako chote kimelenga mahala au sehemu moja bila ya kutapakaza ili uweze kupata kidonge .
- Utaenedelea hivi kwa kujaza karai nafasi yote zikigeuka rangi ya kuiva, unazigeuza upande wa pili paka umalize zikiwiva kwa rangi nzuri.
- Tumia sahani ukiwa umetandaza karatasi za jikoni kuweza kuchuja mafuta baada ya kuchoma. Kisha badilisha kwenye sahani au bakuli nyengine, tayari kuliwa.
Kidokezo;
Huliwa kwa chatini ya aina yoyote, na unapochoma ukiona unga haupandi juu basi lazima kuna itilafu.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha

assalam aleykum unga wa
assalam aleykum unga wa dengu unaitwaje kwa english
Wa 'alaykumus-salaam wa
Wa 'alaykumus-salaam wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuh.
Unga wa dengu unaitwa kwa Kiingereza 'Gram Flour'
Kula kwa siha na afya.