Kachori

Kachori

 

Vipimo

 

Viazi (mbatata) - 2lb

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi - Kijiko 1 cha chakula

Chumvi - Kijiko 1 cha chakula

Pilipili ya kusaga - kutegemea na unavyoipenda

Ndimu - 1

Mafuta ya kupikia

Unga wa dengu au Ngano - Kiasi.

 

Namna ya kutayarisha na kupika

  1. Chemsha viazi  mpaka viwive, kisha vitoe maganda na uviweka ndani ya bakuli.
  2. Vipondeponde kwa mkono mpaka viwe laini.
  3. Saga thomu na tangawizi kisha changanya na viazi.
  4. Weka chumvi, ndimu na pilipili ya unga, changanya vizuri kisha uonje, unaweza kuongeza viungo hivi kwa kadri ya mapenzi yako.
  5. Tengeneza madonge ya duara uyapange katika tray.
  6. Vuruga unga  wa dengu au ngano kwa maji uwe mwepesi kidogo.
  7. Weka mafuta ya kupikia ndani ya karai na uliweke kwenye moto.
  8. Chovya madonge  kwenye unga na uyatose kwenye mafuta ya moto. (Uchomaji wake ni kama kuchoma bajia)
  9. Wacha kachori  zibadilike rangi kuwa ya njano na uzitoe kwenye mafuta.
  10. Weka Kachori  kwenye sahani zipoe tayari kwa kuliwa.

 

Kidokezo.

 

Ni nzuri sana kuliwa kwa chatne, au kwa kuchanganywa kwenye mix ya bajia na mbatata za rojo.

 

 

 

Share