Uzazi: Ametia Niyyah Kufanya 'Ibaadah Zote Ramadhwaan Lakini Ameshindwa Kwa Uzito

SWALI:

Assalaam aleykum warahmatullaahi wabarakaatu,namshukuru allah azzah wajallah kwa kutuweka mpaka kuufikia mwezi huu mtukufu wa ramadhan,Mungu atawalipa kwa mema yote na kazi ngumu munazokabiliana nazo,Ameen,mimi nilitia nia kufanya ibada zote katika mwezi huu mtukufu khaswa kusoma qur'aan kwa wingi na kuswali qiyaamullayli,lakini kabla ya kuingia mwezi huu mtukufu nimepata neema ya uja uzito na ninasumbuliwa sana na kichwa,najibidiisha kufunga lakini nashindwa kusoma qur'aan na swala ya usiku,pia nina mtoto mdogo hunisumua sana usiku,na qur'aan husoma ninapoamka kuswali fajri kidogo,nini hukumu yangu,naomba munisaidie ndugi zangu,wabillahi tawfiq.

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Hiyo ni dalili ya mapenzi ya kufanya ibada, ni jambo la kufurahisha na kutia iymaan. Lakini inapasa utambue yafuatayo:

Kwanza ni kwamba hakuna ubaya wowote madamu umeshindwa kutekeleza ibada zako ulizoziwekea nia kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Hamkalifishi mja ila kwa uwezo wake. Nawe basi haipasi kujikalifisha kwani kufanya hivyo kutazidi kukuletea madhara ya afya yako. Inatosha kwamba ni

 

 ((لاَ يُكَلِّفُ اللّهُ نَفْسًا إِلاَّ وُسْعَهَا لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ ))

((Allaah Haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo. Faida ya iliyoyachuma ni yake, na hasara ya iliyoyachuma ni juu yake pia)) [Al-Baqarah: 286]

 

Pili madamu ni mja mzito, tayari umeshapewa ruhusa ya kutokufunga.

Juu ya hivyo maadamu ulitia Niyyah ya kufanya jambo jema basi hata kama umeshindwa tayari utakuwa umeshapata thawabu moja ya kila kitendo. Hii kutokana na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

((إن الله كتب الحسنات والسيئات , ثم بين ذلك , فمن هم بحسنة فلم يعملها كتبها الله له عنده حسنة كاملة فإن هو هم بها فعملها كتبها الله له عنده عشر حسنات , إلى سبعمائة ضعف , إلى أضعاف كثيرة , ومن هم بسيئة فلم يعملها , كتبها الله عنده حسنة كاملة , فإن هو هم بها فعملها كتبها الله له سيئة واحدة )) متفق عليه ،  

((Allaah Ameandika mema na mabaya. Kisha Akayabainisha. Basi atakayetia nia kutenda jema kisha asilifanye, ataandikiwa jema moja kamili. Atakapofanya hima na akalitenda, ataandikiwa mema kumi hadi kuzidi mia saba na ziada nyingi. Na atakayetia nia kufanya kitendo kibaya kisha asikifanye, ataandikiwa jema moja kamili. Atakapokifanya  ataandikiwa dhambi moja)) [Al-Bukhaariy ya Muslim]

  

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share