029 - Kisomo Chake (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Swalah Za 'Iyd Mbili - Sifa Ya Swalah Ya Mtume
9- SWALAH ZA 'IYD MBILI
"Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)akisoma (mara nyingine) katika Rakaa ya kwanza
سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى
Sabbihisma Rabbikal A’laa
((Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa)) [Al-A'laa 87: 19], na katika Rakaa ya pili:
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ
Hal Ataaka Hadiythul Ghaashiyah
((Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?)) [88: 26] [1]. Na mara nyingine "alikuwa akisoma katika hizo Rakaa mbili:
ق وَالْقُرْآنِ الْمَجِيدِ
Qaaf Wal Qur-aanil Majiyd
((Qaaf, Naapa kwa Qur-aan Tukufu))[Qaaf 50: 45], na
اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانشَقَّ الْقَمَرُ
Iqtarabatis Saa’atu wan-shaqqal Qamar
((Saa imekaribia na mwezi umepasuka)) [Al-Qamar 54: 55][2].
- Login or register to post comments
- Email this page
