Aya Katika Surat Faatwir Ina Maana Gani?

SWALI:

I have a question that maybe most of the people want to know  about. Its about the Quran . Well i know arabic and i can read the Quran but i dont understand what it means i just read. Sometimes i  wonder why is this Surah brought down. 

I  read an article saying that one man was about

to die, the Malaika was there want to take out his roh, so there was  someone with him in the room, so the Malaika told the person can you  move because i want to take out his roh, the person said no, i cant  leave him, he was there for me  and i cant leave him, so the Malaikas struggled to take out his roh while the person is there watching. At the end i knew that that person is the Quran, its the one  who will be there for you because it will tell you that you didnt

leave me and i wont leave you.

 

UFAFANUZI ULIOHITAJIKA KUTOKA ALHIDAAYA ILI SWALI LIWEZE KUJIBIWA:

Tunahitaji kujua kama uliyotaja ni Tafsiyr ya Surah au Aya, na kama ndio, tafadhali tujulishe ni Surah gani na Aya gani ili tuweze kuhakikisha usahihi wake na kuweza kujibu Swali lako Insha Allaah.

Majibu ya muulizaji ni:

 

Assalamu Alaikum

   The Aya that i really want to know is Suratul Fater, Ayya 28  

 (( إنما يخشى الله من عباده العلماء))     فاطر : 28

((Kwa hakika wanao mcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni)) [Faatwir:28].  

 

 

  

JIBU:

BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu wa Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa  Aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa Ba’ad

Baada ya kufanya utafiti wa aya hiyo hatukuona maelezo hayo uliyotaja kuhusu mtu aliyekuwa anakata roho, bali maelezo yenye maana ya aya hiyo ni kama ifuatavyo:

 

((إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاء ))

((Kwa hakika wanaomcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja Wake ni wanazuoni )) [Faatwir: 28]

Nao ni wale wenye elimu na wenye kumkhofu Allaah kama Apasavyo kukhofiwa kwa sababu kila anapokuwa mtu ana elimu ya kumtambua Mola Mtukufu, Mwenye nguvu, Mwenye ujuzi, Mwenye sifa zilizokamilika na Mwenye majina matukufu ndipo anapokuwa anazidi kuwa na khofu Naye.

Ibn 'Abbaas amesema kuhusu aya hii:

"Miongoni mwa waja wanaomjua Ar-Rahmaan ni yule ambaye hamshirikishi na chochote katika kumuabudu. Na ni mwenye kukubali yaliyo halali Aliyohalalisha na kukubali kuepukana na yaliyo haramu Aliyoharamisha Allaah  سبحانه  وتعالى. Ni mtiifu wa amri zote na ana yakini kuwa ataonana Naye na kuwa atasimamishwa mbele Yake kuhesabiwa vitendo vyake".

Hasan Al Basriy amesema:

"Mtu mwenye elimu ni yule mwenye kumkhofu Ar-Rahmaan kwa mambo yasiyoonekana, na mwenye kupenda yale ambayo Allaah سبحانه وتعالى Anamtaka ayafanye na mwenye kujiepusha na yale ambayo yanamghadhibisha Allaah" Kisha Hasan Al Basriy akasoma:

((إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاء إِنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ غَفُورٌ))

Kwa hakika wanaomcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja Wake ni wanazuoni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe)) [Faatwir: 28] 

Sufyaan Ath-Thawariy amesimulia kutoka kwa Abu Hayyaan At-Taymi kutoka kwa mtu aliyesema: "Iilikuwa ikisemekana kuwa wenye elimu ni aina tatu; (kwanza) mwenye kumjua Allaah  سبحانه وتعالى na amri Zake (pili) mwenye kumjua Allaah  سبحانه وتعالى lakini hajui amri Zake (tatu) mwenye kujua amri Za Allaahسبحانه وتعالى lakini hamjui Allaah سبحانه وتعالى .   

Mwenye kumjua Allaah  سبحانه وتعالىna amri Zake ndiye mwenye kumkhofu Allaah سبحانه وتعالى na mipaka Yake pamoja na aliyofaridhishiwa. Mwenye kumjua Allaah  سبحانه  وتعالىlakini hajui amri Zake ni mwenye kumkhofu Allaah lakini hajui mipaka yake na aliyofaridhishiwa. Mwenye kujua amri za Allaah سبحانه وتعالى lakini hamjui Allaah سبحانه وتعالى ni mwenye kujua mipaka na aliyofaridhishiwa lakini hamkhofu Allaah سبحانه وتعالى.  [Ibn Kathiyr :8:145-146]

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share