Kutoa Mimba Ikiwa Ikiachwa, Mtoto Atakuwa Mgonjwa Au Kufariki Baadaye

SWALI:

 

Asalam laikum.

Naomba kuliza hivi inafa kwa mja mzito kuenda hospital kufanya ultrasound kujua kwamba ni mtoto wa kike au wa kiume na pia mara nyengine huwa wanambiwa kama mtoto mgonjwa kutokana damu zenu hazikubaliana husababisha sumu kwa mtoto kupata maradh au kufa sasa hushauriwa kuzitoa au waendelea kukaa nazo wakitaka je hii inafaa kutoa mimba hali kama hii?

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kutoa mimba.

Hakika ni kuwa siku hizi imekuwa ni biashara kwa madaktari hasa katika nchi zetu za Afrika na nyinginezo kuwatishia wagonjwa ili wapate biashara au kufanya upasuaji ili wapate pato kubwa zaidi.

 

 

Uislamu umeweka mikakati yake katika kila jambo. Ikiwa mzazi ataambiwa na daktari mtaalamu na aliyebobea katika suala la magonjwa kwa mzazi na mtoto bila kuwepo tashwishi ya aina yoyote ile itafaa kwa mzazi kukubali kutolewa mimba ili aokolewe mama. Hata hivyo, wazazi wanatakiwa waende kwa daktari wataalamu katika fani hiyo na ikiwa kutakuwepo na daktari Muislamu mcha Mungu itabidi muende kwake. Kufanya hivyo kunaingia katika msingi wa Kiislamu: “Akhaffu adhw-Dhwararayn – uhafifu katika madhara mawili”.

 

Ama kuhusu kujua mtoto gani ingia katika kiungo kifuatacho:

 

Kujua Aina Ya Mtoto Aliyeko Tumboni Kwa Ultra Sound Kabla Hajazaliwa

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share