Inafaa Kufunga Ndoa Na Mtoto Wa Dada Ambaye Ndugu Kwa Baba?

SWALI:

 

Assalam aleykum. Inshallaah mungu akulipeni kheri duniani na akhera kwa msaada wenu.amma baad. Kuna swala lani tatiza sana...Hal ina juzu mtu akiwa ana dadake kwa baba lakini hawaku lelewa pamoja na kila moja kalelewa na mamake katika nyumba tofauti. Hal ina juzu kufunga ndoa na mtoto wa dadake? Shukran na Allah awajaze kher

 


 

 

JIBU:

 

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kufunga ndoa na mtoto wa dada ambaye ndugu kwa baba.

Ndugu yako ni ndugu yako kisheria akiwa ni kwa baba na mama (shaqiqi), au kwa baba tu au kwa mama tu. Na undugu huo hauondoki kisheria ikiwa mmelelewa pamoja au mbali mbali.

 

Ikiwa hali ni hiyo sheria imekuekea kuwa huwezi kumuoa binti ya dadako kwa hali yoyote ile. Na Allaah Aliyetukuka Amesema kwa uwazi kabisa: “Wameharamishwa kwenu mama zenu … na mabinti wa dada …” (An-Nisaa: 23).

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share