Bilaal (رضي الله عنه) Alibaguliwa Hadi Kutokupewa Mke?

 

Bilaal (رضي الله عنه) Alibaguliwa Hadi Kutokupewa Mke?

 Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Kwanza namshukuru Allah kwa sababu ndie anaestahiki kushukuriwa pili nawapongeza kwa misaada yenu munayotusaidia suala langu ni hili: nilikuwa napenda kujua kama swahaba Bilaal ibn Rabaah aliowa na alibahatika kupata watoto kwa sababu kuna watu wanosema mtu mweusi hana thamani yoyote katika uislamu: wakimaanisha kwamba bilali alibaguliwa hakupewa mke katika wakati mtume kwa sababu alikua mweusi na wanasema alikufa na nyege kama punda je kuna ukweli wowote kuhusu maneno yao hao?

 

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho 

 

 

 

Hakika ni kuwa wapo watu ambao kazi yao ni kuwashutumu Maswahaba kwa namna moja au nyingine au kuwapa sifa mbaya kwa njia tofauti. Hilo ni jambo ovu kabisa kuzua mambo ambayo hayapo.

 

 

Bilaal (Radhwiya Allaahu 'anhu) alioa mke wakati wa uhai wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na aliyemkomboa Bilaal (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na kumtoa katika utumwa alikuwa ni Abu Bakr Asw-Swiddiyq (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye alikuwa ni Mwarabu. Kwa hiyo hayo madai yaliyotolewa ni ya kipuuzi hayana ukweli wowote.

 

Soma Historia ya maisha ya Bilaal (Radhwiya Allaahu ‘anhu) katika kiungo kifuatacho:

 

 

Bilaal Bin Rabaah (رضي الله عنه)

 

 

Pia kuna mawaidha kumhusu Swahaba huyo na wengi wengineo ndani ya Alhidaaya.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share