Vipi Kuondosha Wasiwasi Wa Mashaka Ya Najsi

SWALI:

Asalam alaikum ndugu waislamu

Mbele yayote naomba Mola abariki kazi munazozifanya na awalipeni. Mimi ninatatizo ambalo linanisumbua mpaka wakati mwengine huwa nasikia kama kichwa kinanizunguuka, na tatizo hili nilamashaka,yaani naweza nikatoka chooni nikiwa nilisha jisafisha,ama nikamaliza kutawaza kabla yakusali lakini bado nikawa na mashaka kwamba kuna maali ambapo bado kuna uchafu ama hapakufika maji,na hizo mashaka zinanisumbua mpaka nakosa amani, vile vile wakati wakujitwaharisha.katika hali kama hiyi sijuwi niwe nafanya nini? Pia watoto wangu wanaweza kunya ama kukojowa mkojo ukaruka maali pengi ambapo sioni maali pengine ambapo ule mkojo umerukia, naweza nikawabadili nepi na nikawafuta lakini bado nikawa namashaka kuwa kunamaali pengine ambapo bado kuna ile najisi  katika maali ambapo ule mkojo ulirukia ama mavi  hata kama siioni(mkojo au mavi) ila nahisi tu kama kunamaali ambapo bado kuna najisi ila sijuwi ni wapi  ,nakama nichumbani njo walirushia mkojo ama mavi,huwa nakuwa na wasiwasi kwamba kuna maali ambapo bado kuna najisi hata kama sioni iyo maali  ,nini chakufanya ikitokea hali kama hiyo? Nikisualia iyo maali ama nguo ambazo nilikuwa navaa ule wakati na ambazo pia nina wasiwasi nazo sala inakubaliwa ama haikubaliwi?

 




 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Tunamuomba Allah Atubariki sote na Atupe hima katika Dini Yake. Wasiwasi mara nyingi unatokana na shetani aliyelaaniwa, kwani Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema: “Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannaas. Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu, Kutokana na majini na wanadamu” (114: 4 – 6).

Hivyo unapopata pepesi za shetani au wasiwasi kama huo unatakiwa useme Audhu Billaahi minash Shaytwaanir Rajiym (Najilinda kwa Allah kutokana na shetani aliye laaniwa). Bila ya shaka wasiwasi huo utaondoka. Usimpe shetani nafasi ya kukuchezea. Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema:

Na uchochezi wa Shetani ukikuchochea basi omba ulinzi wa Allah. Hakika Yeye ni Msikizi, Mjuzi. Hakika wale wamchao Mungu, zinapowagusa pepesi za Shetani, mara huzindukana na hapo huwa wenye kuiona haki” (7: 200 – 201).

Kwa kawaida shetani anataka kukushughulisha kwa mambo ambayo si ya msingi ili kukupotezea wakati wako ambao ni muhimu au ufanye jambo ambalo si muhimu.

Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) Haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kinachoweza nafsi hiyo. Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) Hakuweka uzito wowote katika Dini (22: 78).

Unachotakiwa kuondoa katika najisi ni ile unayoiona, ile ambayo hujaiona au kuisikia harufu basi si juu yako kujitia wasiwasi. Toa wasiwasi wote juu ya najisi kama hizo mpaka ujue uhakika wake. Wakati mmoja ‘Umar ibn al-Khatwtwaab (Radhiya Allaahu 'anhu) alikuwa anapita na mwenzake mara yakamwagwa maji kutoka juu ya nyumba. Yule bwana akaanza kuuliza kama yale maji ni ya najisi, ‘Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) alimkemea kuhusu hilo na akamkanya kuuliza, kwani kufanya hivyo ni kujitia katika mashaka.

Kwa manufaa zaidi bonyeza viungo vifuatavyo:

Na Allah Anajua zaidi

 

Share